Toleo jipya:
Na Henry Kazula,
Mtaalamu wa Sayansi ya Mazingira,
"Nelson Mandela African Institution of Science and Technology, Arusha-Tanzania"
Mwandishi, Msemaji wa hadhara na mhamasishaji wa mabadiliko
__________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________
Na Henry Kazula,
Mtaalamu wa Sayansi ya Mazingira,
"Nelson Mandela African Institution of Science and Technology, Arusha-Tanzania"
Mwandishi, Msemaji wa hadhara na mhamasishaji wa mabadiliko
__________________________________________________________________________________
__________________________________________________________________________________
Photo:http://www.eecuk.co.uk/energy-efficiency-climate-change-and-the-city-of-london/ |
Kutokana
na taarifa ya jopo la wataalam wa mabadiliko ya tabianchi
duniani-“Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC)” wanasema kuwa, mabadiliko
ya hali hewa husemekana kuwa ni hali yoyote inayopelekea kubadilika kwa tabianchi na ya dunia kwa ujumla wake, hii ni kutokana na visababishi asilia ukijumisha
shughuli mbali mbali za binadamu.
Mabadiliko
ya tabianchi na dunia kwa ujumla hujumisha viashiria kama kuongezeka kwa joto
duniani (...husababisha kuyeyuka kwa barafu), kuongezeka kwa kina cha bahari
(huatarisha kutoweka kwa visiwa mbali mbali duniani),ukame na mvua zisizokuwa
na utaratibu,mafuriko.
Kuna
madhara* mbali mbali yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi-hasa kwa binadamu
ambaye ni mchangiaji wa mabadiliko hayo;
· *Upungufu
wa mvua na mafuriko husababisha tatizo la upatikanaji wa chakula-hivyo gharama za chakula kuongezeka
· *Kuibuka
kwa magonjwa -mfano kuongezeka kwa joto kumepekea kuenea kwa ugonjwa wa Malaria
kwenye maeneo yaliyokuwa na baridi na hayakuwa na ugonjwa huo hapo awali
· *Kuteteresha
uchumi wa Nchi- hasa kutokeapo majanga yasababishwayo na mabadiliko ya hali ya
hewa, mfano: mafuriko huaribu miundo mbinu ya nchi iliyo muhimu kwa kukuza
uchumi, pia fedha za maendeleo hutumika katika majanga kusaidia wahanga
· *Kupotea
kwa viumbe kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa katika sehemu husika
* Nchi masikini na zinazoendelea zipo kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi.
Kwa
kipindi kirefu kumekuwa na marumbano ya hapa na pale kuhusu chanzo cha
mabadiliko ya tabianchi, binadamu amekuwa akinyooshewa kidole kuwa ni
chanzo kikubwa cha mabadiliko hayo kutokana na shughuli mbali mbali za kijamii
na kiuchumi.
Takwimu
za kihistoria zinaeleza kuwa kwa kipindi cha miaka elfu kumi iliyopita hali ya hewa na tabianchi haikuwa na
mabadiliko yoyote, ikimaanisha kuwa ilikuwa kawaida, ingawaje kuanzia hapo hali
ya tabia/hewa imekuwa ikipitia mabadiliko ya hapa na pale.”Swali linakuja, nani
amechangia mabadiliko hayo hadi sasa?” kama nilivyoeleza awali, kuna visababishi
asilia na shughuli za binadamu.
Kuna kila
sababu kuwa shughuli za binadamu zimechangia kwa kiasi kikubwa katika
mabadiliko hayo na haya tunayoyaona.Ondea mbali visababishi asilia ambavyo naweza kusema vilikuwepo tangu kuwepo
kwa dunia.
Binadamu
ameingilia kwa kiasi kikubwa mfumo wa hali ya hewa ujumuishao; anga la hewa,
maji (bahari na vyanzo vyake),barafu,ardhi na eneo la viumbe uhai.
Ingawaje
mfumo wa hali ya hewa huendeshwa pia na visababishi
asilia kama vile mripuko wa volcano,
kubadilika kwa miozi ya jua ifikiayo uso wa dunia, muingiliano wa bahari na
anga la hewa, mikondo ya bahari iletayo baridi na joto nchi kavu na kubadilika
kwa mizunguko ya dunia katika kulizunguka jua kutokana na kani mvutano iliyopo
kati yake na mwezi na sayari nyingine.
Shughuli
mbali mbali za binadamu zilizo sanjari na uvumbuzi na kukua kwa viwanda duniani
kumepelekea kuongezeka kwa joto kama inavyoripotiwa na wataalamu wa masuala ya
hali hewa duniani-IPCC.
Ongezeko
la joto duniani la Sentigredi 2 kwa karne hii ya 21 limeifanya dunia kuwa katika vipindi hatarishi
viambanavyo na majanga mbali mbali.Ongezeko hilo linalosemekana kusababishwa na
ongezeko la takribani 400ppm la hewa ukaa-kabonidioxide gesi (CO2) inayokumbatia joto la
dunia mara tu gesi hii ichukuapo joto kutoka kwenye mionzi ya jua hivyo kufanya joto
kuzidi kubaki katika uso wa dunia.Inakadiriwa kuwa hewa hiyo itaongezeka kufikia 550ppm (mara mbili zaidi kabla ya mapinduzi ya viwanda) na kupelekea ongezeko la joto duniani la Sentigredi 3 kufikia 2050. Ongezeko hii ni la hatari kama juhudi za makusudi na za pamoja hazitachukuliwa kupunguza hewa ukaa.
Mtu aweza
kuuliza, nini hupelekea kuongezeka kwa hewa ukaa? Jibu ni rahisi sana ndugu
msomaji: shughuli za binadamu kama uzalishwaji wa nishati kupitia makaa ya
mawe, uchomaji misitu, kubadilisha uoto wa asili kuwa makazi na viawanda,
ukataji miti, shughuli za viwanda, vyombo vya usafiri kwa kuunguza mafuta
n.k.Ukiangalia kwa makini utaona kuwa shughuli za kuinua uchumi zinachangia kwa
kiasi kikubwa kwa mabadiliko ya tabia ya nchi.Hii ndiyo sababu mataifa makubwa
yaliyojiimarisha kiuchumi yanakwepa kuchangia juhudi za kupunguza ongezeko la
hewa ukaa duniani na kuhamasisha nchi masikini na zinazoendelea kuwa mstari wa
mbele kupunguza ongezeko la hewa ukaa.
Ndugu
msomaji, unaweza kufikiri kuwa uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira katika
sehemu nyingine duniani hauleti madhara kwa Taifa lako…madhara yapo, tena ni
makubwa kwa sababu hewa ipo katika mzunguko na hubeba hewa mbaya kutoka
eneo moja hadi lingine.Hivyo, hatuwezi kujitenga katika juhudi za kumbana na kupunguza
hewa ukaa.
Kila Taifa lina wajibu wa kupambana kudhibiti ongezeko la hewa ukaa kabla ya hali ya hatari haijatufikia...naweka msisitizo kwa mataifa makubwa yaliyojiimarisha kiuchumi kutokana na viwanda kuwa mstari wa mbele kupunguza ongezeko la hewa ukaa na si kutoa misaada kwa nchi masikini kupambana na tatizo wakati nchi hizo kubwa zikiendelea kufanya uchafuzi bila kuchukua hatua madhubuti za kupunguza tatizo.
Bila
shaka ,kwa kiasi chake umeona ni jinsi gani binadamu anavyochangia mabadiliko
ya tabianchi.
Tukutane
wakati mwingine katika ukurasa huu ujue zaidi kuhusu “mbinu za pamoja kupunguza hewa ukaa na gesi nyingine zinazochafua
anga”
"Mabadiliko huanza na mimi na wewe"
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Rejea:
Burroughs,W.J.(2007). Climate Change.A multidisciplinary Approach.2nd edition. United Kingdom:University Press,Cambridge.
IPCC,(2007).Climate Change 2007:Scientific Basis,Cambridge,UK:Cambridge University Press.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni