Picha:http://lifeinzd.com/why-telling-the-truth-sucks-and-why-its-awesome-a-case-study/ |
Umewahi kujiuliza kama mambo uyaonayo na kuyasikia ni kweli?
Kila siku tunaona na kusikia wengine wakitueleza masula mbali mbali kutuhusu au
kuwahusu wao na kukurupuka katika kuyafanyia kazi bila kufanya utafiti wa kina.Soma hii pia.
Lakini, ni mara
ngapi tumejiuliza kama masuala hayo ni kweli kabla ya kuchukua hatua za makusudi za utekelezaji? Pia, ni nini hutuaminisha kuwa mambo hayo ni kweli? Au
unajuaje kama makala hii ninayokuandikia uisome sasa ni kweli?
Kupitia maswali hayo ya msingi ni vyema nikakushirikisha
mtazamo wenye msaada wa karibu kutoka kwa Wabuddha;
“Believe nothing. No matter
where you read it, or who said it, even if I have said it, unless it agrees
with your own reason and your own common sense.” …kwa tafsiri isiyo rasmi inamaanisha kuwa-
“Usiamini chochote. Bila kujali umesoma mahali au kupitia mtu fulani na hata
kama nimesema, isipokuwa tu kinaendana/kinashabihiana
na upeo wako wa kufikiri na akili yako ya kawaida katika kutoa maamuzi". Msisitizo
umewekwa kwenye upeo wa kufikiri na uwezo wa kawaida katika kutoa maaamuzi.
Je, unafanyaje kuboresha au kunoa upeo wako wa kufikiri na
uwezo wako katika kutoa maamuzi sahihi kwa wakati husika? Kupitia makala zetu
kuhusu mtazamo utaona kuwa tunasisitiza kuhusu Kujielimisha Kwanza! hii ikiwa
ni njia pekee ya kujua ukweli wa mambo kama Mwl.J.K.Nyerere alivyoanisha katika
kijitabu chake cha TUJISAHIHISHE.Kuelekea kujua ukweli wa mambo tunaboresha na
kunoa upeo wetu wa kufikiri na ufahamu katika kutoa maamuzi sahihi na yenye tija.
Sioni haja ya kuficha au kuzunguka sana, la msingi ni kusoma
mambo mengi kupitia vitabu,majarida yenye tija na kusikiliza hotuba mbali mbali sambamba na kulinganisha mawazo ya watu tofauti, changanya na uwezo wako wa kupambanua mambo kuhusu
uhalisia wa jambo fulani katika maisha, mwisho kuweza kutofautisha mchele na pumba.
Pia jifunze jinsi ya kuunganisha matukio tofauti tofauti ili kukufikisha katika jambo au suala unalotaka kujua undani wake.Kupitia njia hizi unaweza kuwa mpelelezi wa kuijua kweli iliyo suluhisho la kututoa njia panda, na mwisho wa yote unaweza
kutumia uzoefu huu kutatua matatizo mbali mbali ndani ya jamii.
Usikubali kudanganywa!... kwa maana anayekudanganya hukuchukulia wewe kama mtu usiyeweza kutumia upeo wake vizuri katika kupambanua mambo.Hivyo usije naswa katika mtego wa kudanganywa...tumia njia tajwa kufuatilia na kuujua ukweli wa mambo.
Kuna faida kem kem za kujijengea tabia ya kupeleleza na
kujua ukweli kuhusu jambo au mambo fulani, kuanisha chache;
1.KUEPUKA MIGOGORO ISIYO YA LAZIMA
2.KUTATUA MATATIZO KIRAHISI BILA UPENDELEO WA UPANDE FULANI
3.KUJIONGEZEA WIGO WA KUFAHAMU MAMBO MENGI YENYE TIJA KWA
MAISHA YETU
4.HUTUPELEKEA KUWA NA MTAZAMO CHANYA WA MAISHA NA KUWAJUA
WENGINE KIUNDANI BILA KULETA UGOMVI
5.KUWA NA UHURU WA NAFSI ISIYO NA MAWAA
6.KUWA NA FURAHA ILIYO MUHIMU KWA AFYA
7.KUEPUKA MSONGO WA MAWAZO USABABISHWAO NA KUTOFAHAMU UNDANI
WA JAMBO FULANI
8.KUONDOKANA NA ADUI WA MAENDELEO- UJINGA
9. KUJITOA KATIKA UELEWA WA NJIA PANDA.
Jielimishe Kwanza! Jifunze na utafute kuijua kweli itakuweka huru!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza! SE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni