1.Boresha
ujuzi wako wa kazi kwa kujiendeleza kwa siri ukilenga kuwa mfanyakazi makini
mwenye mbinu stahiki za kazi. Kwa hatua hii utajiongezea uthamani sana katika
eneo lako la kazi. Itafika wakati utamfanya mwajiri akuone ni wa thamani hivyo
atajitajihidi asikupoteze. Ikifika hatua hii: Unaweza kujipangia aina ya
mshahara kulingana na ubora ndani ya ajira husika.
2.Usionyeshe
udhaifu wako kwa mwajiri. Usionyeshe kuwa unabembeleza sana ajira yake,
ukifanya hivyo ni rahisi sana kutumikishwa kama mtumwa kwa sababu umeonyesha
una dhiki.
3.Onyesha
uwezo au kipaji chako kwa kadri uwezavyo. Kama unakumbuka, moja ya athari za
utumwa wa kisasa ni kushindwa kuonyesha kipaji chako…hakuna mazingira rafiki ya
utendaji kazi! Tumia kila mbinu kuhakikisha kipaji chako na uwezo wako wa
kipekee unaonekana katika mazingira ya kazi. Ukifanikiwa, unganisha na mbinu
namba 1 kujiongezea ubora zaidi katika kazi.
4.Acha
kunung’unika chini chini! tenda, onyesha hisia zako kwa vitendo ukihitaji kuona
mazingira rafiki ya kazi.Mweleze mwajiri wako kuwa hujapendezwa na mazingira
yanayoendelea katika kazi.Wafanyakazi wengi wamekuwa ni waoga kuwaeleza waajiri
wao yao ya moyoni kuhusu ujira waupato ukilinganisha na utendaji…wengi
hawaridhiki na vipato vyao, wananung’unika chini kwa chini.Ondoa hofu! Ni
wajibu na haki yako kujadiliana
na mwajiri kuhusu ujira ili kuboresha
utendaji kazi.
5.Ungana
na kikundi cha wapinga “utumwa wa kisasa” katika maeneo ya kazi. Sauti ya wengi
ina nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko.
6.Tambua
wajibu wako kwa kuhitaji “mpango wa kazi
na majukumu kimaandishi” kutoka kwa mwajiri. Hakikisha unajiridhisha mapema
kabla ya kuanza kazi. Majukumu uliyopewa yaendane na ujuzi ulio nao, pia
yazingatie kipato unachopata.
7.Jielimishe
zaidi kuhusu ajira na kanuni zake, haki za wafanyakazi kupitia vyombo mbali
mbali vya habari.
8.Usifanye kazi kwa mazoea. Jitahidi
kuwa mtu wa mabadiliko ukijiongezea uthamani katika soko la ajira.
Tukutakie kila la heri katika kujikomboa na utumwa wa kisasa katika maeneo rasmi ya kazi.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni