Picha: alexrister1.wordpress.com |
Neno “kwanini” au "why" kwa lugha ya Kiingereza
ni la udadisi na uvumbuzi pia ni neno la kutaka kujua kulikoni. Hutusaidia pia
kuweza “kujua ukweli wa mambo”-Kujielimisha!
Hivyo kuweza kujua maana halisi ya mambo yanayotokea, yanayoendelea na mwisho
kutoa maamuzi yaliyo sahihi kwa asilimia kubwa. Pia ni neno la msingi
Kibiashara hasa wakati wa kuwasilisha bidhaa au huduma kwa wateja katika lugha
igusayo hisia na kuteka soko la biashara.
Kwa bahati mbaya, nasikitika kusema kuwa
ni mara chache tumekuwa na utamaduni wa kutumia neno hilo la msingi katika
maisha yetu ya kila siku. Hii ni kwa sababu tunavutika haraka na neno “nini” -“what”, yaani tunavutika haraka na mambo
yanayotokea na kuonekana, hivyo kuyafanyia kazi haraka bila kujua ni “kwanini” yametokea au yapo kama yaliyo.
Kwa bahati nzuri, maktaba yangu kuna
kitabu nilichowahi kukisoma bila kuchoka, kinahamasisha kuendelea kusoma mara
kwa mara; ni cha mwandishi, mhamasishaji na msemaji wa hadhara Simon Sinek kiitwacho-“Start With Why”-“Anza na Kwanini” kwa
tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi. Nakushauri kitafute kitabu hicho usome,
utajua ni “kwanini” kuanza na “kwanini” kuna faida katika kuwasiliana
kibiashara, kutoa maamuzi sahihi ya maisha yetu na kujua ukweli wa mambo.
Ndani ya kitabu hicho, Sinek anasisitiza
juu ya kuanza kwa kujiuliza “kwanini”
katika kutoa maamuzi ya kibiashara na maisha kwa ujumla. Ameanisha hivyo kwa
kutumia duara liitwalo “The Golden cycle”
lenye maneno “why”, “how” na “what” yaani “kwanini”, “kwa
jinsi gani” na “ nini”.
Katika kujiuliza maswali ya
msingi ni vyema kuanza na “kwa nini”,
nawe waweza kuniuliza “kwa nini” tuanze na “kwa nini”? TUKUTANE SIKU KAMA YA LEO UTAZIJUA SABABU HIZO KWA KINA.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni