Picha: alexrister1.wordpress.com
Katika kujiuliza maswali ya msingi ni
vyema kuanza na “kwa nini”, nawe waweza
kuniuliza “kwa nini” tuanze na “kwa nini”? Naweza kutoa sababu za kufanya
hivyo na kukuhamasisha kujijengea utamaduni huo kama ifuatavyo;
1. Kuanza na “kwanini” katika lugha ya Biashara: Utajua
sababu ya wewe kutoa maamuzi na kuwaaminisha wengine kuamini unavyo amini.
Simon Sinek ananisaidia kutoa sababu ya kuanza na “kwanini” katika kufikisha ujumbe wa kibiashara kwa wateja-
nanukuu; “People
don't
buy what you do; people buy why you do it”.
Katika
tafsiri ya lugha ya Kiswahili isiyo rasmi -“watu hawanunui nini unafanya, ila hununua kwa nini unafanya ufanyavyo.
2. Kuanza na “kwanini” katika kutoa maamuzi sahihi na yenye tija
Mambo
mbali mbali hujitokeza katika maisha yetu na hutulazimu kutoa maamuzi pia kututoa
njia panda. Tukihoji kwa kutumia neno hilo “kwa
nini”, tunachochea udadisi ulio na kiu ya kutaka kujua zaidi ni kwa njia zipi
tukio fulani limetokea na kutoa maamuzi sahihi.
Neno hilo huonekana kuwa ni dogo lakini
nguvu yake ni kubwa kwa kubadilisha mfumo
wa kawaida wa utendaji-“status quo” na ufikiri wa maisha yetu unaoendena na
mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.
Hivyo basi, ni vyema kujianzishia
utamaduni huu kwa sababu utakubadilisha kimtazamo kwa vile unavyojichukulia katika
maisha na kuboresha uthamani wa bidhaa na huduma (kwa mfanya biashara) na kutoa
majibu sahihi ya maswali na changamoto za maisha ya kila siku.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni