Maisha yetu ya kila siku
tunakumbana na maswahibu mbali mbali yanayopelekea fikra na utashi wetu
kuchukua maamuzi rahisi na wakati mwingine maamuzi magumu sambamba na kutoa
hukumu kwa yatokanayo.
Ukweli mchungu na usio na
kificho ni kuwa, kila siku katika hali yetu ya kibinadamu tunakalia kiti cha heshima cha uhakimu na kutoa hukumu kuwahukumu
wengine isivyo haki na kweli kutokana na
makosa yatokanayo na maamuzi yao; maamuzi rahisi au magumu.
Kuna jambo la msingi la
kuzingatia kwanza ikiwa tupo kwenye kiti cha kutoa hukumu; ni la kiimani, Sawa!
(kama inayovyoaminiwa na baadhi ya dini) kuwa usihukumu wengine kabla hujahukumiwa-Mungu pekee ndiye wa kuhukumu kwa
haki pia kabla ya kuwahukumu wengine tujichunguze/tujitathmini wenyewe kwanza;
je tu wasafi?, je tupo katika upande wa kutenda haki au upande wa kupenda
kutendewa haki?
Pia, tunapoonyeshea wengine
kidole kwa kuhukumu, itambulike kuwa kuna vidole vitatu vinatonyeshea sisi; hii
ina maana kubwa sana katika uumbaji wa Mungu-tujitathmini sisi kwa kina kwanza kabla
ya kutoa hukumu kwa wengine.
Picha na www.slideshare.net |
Sehemu hii imekuwa ya msingi
sana ili tuweze kutoa hukumu za kibinadamu zilizo za haki na zisizo na mawaa,
ilhali Mungu pekee ndiye anayehukumu kwa Haki na Kweli!
Binadamu kwa asili, tunahukumu
masuala mbali mbali ili kukosoa na kujiridhisha nafsi zetu.Hukumu zetu
huambatana na mtazamo hasi kuhusu wengine, mfano: naweza kuona ndugu au rafiki
yangu amekata mawasiliano na mimi kwa muda mrefu, hii inasumbua akili yangu na
mwisho nashindwa kuchelea kutoa hukumu kwa maneno hasi (bila kujitathmini mimi kwanza kama sijamkwaza)- kuwa ndugu/rafiki
yangu ameanza dharau siku hizi, anajisikia sana, ananionea wivu ameona
nimemzidi kimaisha, yeye ameona kuwa mimi sifai na si wa hadhi yake, ameona
atuendani kiuchumi na mengine mengi; haya ni baadhi tu ya majibu rahisi ya
kupoza hisia ingawaje sijui kama natoa hukumu ya haki na kweli juu yake. Je, ni kweli ipo hivyo? Vipi kama ana matatizo?
Mara ngapi nimefuatilia kujua kuhusu ndugu/rafiki yangu? Ni mfano tu ndugu
hakimu mwenzangu ambao umewahi kunitokea…nimejifunza na ninaendelea kubadilika
kwa hili.Natumaini nawe utafanya juhudi kwa hili.
Makala inayohusiana: Usitoe maamuzi hasi bila kufanya utafiti wakutosha
Sawa, tunaweza kuona ni
jambo jema kwa kufurahisha nafsi zetu na kuwakosoa wengine kwa mapungufu yao
lakini jambo la kuzingatia na la msingi, narudia tena kwa msisitizo; tujitathmini wenyewe kwanza ili hukumu zetu ziendane
na matakwa ya Yule aliye Hakimu wa Kweli na Haki.
Picha na www.pinterest.com |
“Kumpatia mtu silaha asiyohitaji na asiyoweza
kuitumia ni sawa na kutompa kabisa, pia ni hatari; inaweza kumdhuru” –HenryKazula.
Maarifa
kwa wanaohitaji maarifa, pia walioonyesha nia ya kuhitaji maarifa.Onyesha
uhitaji wa maarifa,tutakuelimisha kutumia vizuri maarifa uliyopewa.
Imetayarishwa
na
Mwandishi
wa Kitabu-Mtazamo Wako Ni Upi?
Imetolewa
na
Jielimishe
Kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni