Picha na lauraecpaul.wordpress.com |
Tunaishi katika dunia iliyozungukwa na matatizo kadha wa kadha yaliyo ya asili na mengine ni chanzo cha mwanadamu mwenyewe kwa kudharau mambo yanayoonekana kuwa ni madogo.
Matatizo
yaliyopo huchochea fikra za mwanadamu katika kuelekea kutoa suluhisho au
kutatua matatizo; mwisho wa siku imekuwa
ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku kupambana na kukuna vichwa kutatua
matatizo.
Mtazamo tofauti umejengeka
na kuzoeleka kwa wanajamii katika kuelewa na kutatua matatizo, wengi hutizama matatizo pekee na kukurupuka kutoa
majibu rahisi ya matatizo kwa hisia bila kuyafahamu matatizo yenyewe kwa kina
na kujali chanzo cha matatizo hayo kwa kufanya uchunguzi au utafiti wa kina.Hii
ni sahihi kurejea msemo huu wa Kiswahili-“usiangalie
umeangukia wapi,angalia ulipojikwaa”.
Katika ulimwengu huu tunaoishi kuna matatizo kama
nilivyosema awali; matatizo yana chanzo chake kama ilivyobainishwa na msemo wa
kisayansi katika sheria ya mwanafalsafa Socratic- na
sheria yake ya “law of causality” –“The Law of Cause & Effect states that
absolutely everything happens for a reason.” sheria hii ikiainisha wazi kuwa
kila jambo hutokea kwa sababu maalum.
Tukitupia jicho upande mwingine wa kutoa au kutafuta suluhisho
la matatizo duniani, mwana fisikia maarufu duniani- Albert Einstein anatukumbusha kuwa; “We cannot solve our problems with the same thinking we used when we
created them.” Akimaanisha kuwa matatizo hayapatiwi
suluhisho kwa uelewa wetu ule ule uliotumika kuyatengeneza-hivyo tunahitaji
kufikiri tofauti.
Einstein
anasisitiza tena kwa kujiweka mwenyewe katika kuchunguza na kuelewa matatizo kuwa-“If I had an hour to solve a problem
I'd spend 55 minutes thinking about the problem and 5 minutes thinking about solutions.”-Akimaanisha
kuwa ni vizuri kutumia au kujipatia muda wa kutosha (wa dakika 55) kufikiri na kuelewa
tatizo na hatimaye kutumia muda mchache (wa dakika 5) kutoa suluhisho ikiwa angepata
saa moja kutatua tatizo fulani.
Nikutie
ujasiri ndugu msomaji, hatupaswi kuwa watu wa kulalamika au kukata tamaa
kutokana na matatizo yaliyopo na yanayoendelea kuwepo.Tunapaswa kutumia utashi
au akili binafsi tuliyopewa na Muumba wetu kufikiri na kuyaelewa matatizo kwa kina-hasa chanzo chake kupitia tafiti na
njia mbali mbali zilizotumika na wengine kwa kujielimisha kwanza hatimaye kupata suluhisho sahihi la matatizo
yetu.
Imetayarishwa
na
Mwandishi
wa Kitabu-Mtazamo Wako Ni Upi?
Imetolewa
na
Jielimishe
Kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni