inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumamosi, 21 Machi 2015

MTAZAMO: WENGINE HUFANYA HIVI ILI UWATEGEMEE…

--> 
Picha na seriouslymen.com
Ifahamike kuwa binadamu haishi kama kisiwa; anaishi kwa kutegemea, kutegemewa pia kwa kutegemeana na wengine, pia viumbe hai na visivyo hai.Kusema hivi nakumbuka mwaka 2005-2009 nilipokuwa nikifundisha somo la “Elimu ya Viumbe-Baiolojia” katika mada ya Ikolojia ngazi ya shule za sekondari kuwa; viumbe hai (mimea na wanyama) hutegemeana pia hutegemea viumbe visivyo hai kama hewa, maji, ardhi n.k.Hii hupelekea kuwepo kwa mlishano wenye kutegemeana ili kuishi na kuendeleza kizazi.Napenda kukumbushia tu kuhusu kutegemeana!
Sihitaji kuingia ndani zaidi ya hapo, sipendi kuigeuza safu hii darasa la Baiolojia. Moja kwa moja nianze na safu hii kwa kumlenga binadamu nikidhamilia kurusha mkuki kwa watu wanaopenda wengine wawategemee kupita kiasi ili wawafanye watumwa/mateka wa fikra na hatimaye kupora uhuru wao.


Ndugu msomaji, ikiwa unahusika au huusiki kwa kuwafanya wengine wakutegemee kupita kiasi napenda nikujuze SIRI 10 zilizojificha na zinayoonekana kuwa hali ya kawaida katika maisha ya kila siku. Watu hao wanaoonekana au kujiona wajanja huwafanyia watu wengine yafuatayo kwa kujua au kutokujua ili kuwaweka kwenye mtego wa kuwa watumwa wao kifikra, kimtazamo, kiutendaji na waendelee kuwa tegemezi;

1.               HUWAPATIA WENGINE “Samaki Na Si Nyavu...”
Katika lugha rahisi ni kuwa hawakupatii ujuzi au mbinu au msaada ujikomboe mwenyewe na shida ulizonazo.Hutumia kanuni iliyoainishwa na mwandishi wa 48-Laws of Power akisema;  Never teach them enough so that they can do without you”. Katika tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi-Usiwafundishe vya kutosha ili washindwe kufanya lolote bila ya wewe”
2.           HUTOA MSAADA WA FEDHA KWA DHAMANA YA KITU KINGINE CHA THAMANI WANACHOONA WENGINE (WATUMWA WAO) WANACHO

Ikiwa unapokea msaada wa fedha kutoka kwa mtu wako wa karibu na kuwekewa sharti-nitakupatia fedha unazohitaji ukinipatia…...au “nakupatia hizi hela ila itabidi unipe……” ujue unakaribia kuingia kwenye mdomo wa simba.
3.               HAWAELEZI SIRI YA KUFANIKIWA KWAO
Watu au makundi ya watu wanaopenda uwategemee, hata siku moja hawatoi siri ya kufanikiwa kwao…wataeleza mafanikio yao juu juu tu katika lugha tamu iliyozoeleka na wengi kama kujituma na juhudi binafsi-hivyo watakuambia fanya kazi kwa bidii! Ni vigumu kwao kutoa ile silaha ya kufanikiwa kwao kwa watu wanaowachukulia kuwa watumwa au wategemezi wao.
4.       WANAKUCHAGULIA MARAFIKI
Ikiwa wamekuweka mikononi mwao; yaani unawategemea katika msaada, wataanza kukuchagulia marafiki wa kuambatana nao walio marafiki kwao na kutaka ujitenge na maadui wao au waliowazidi mbinu za kiuchumi.Haijalishi kama una urafiki wa karibu na hao maadui zao, itakulazimu tu ujitenge nao ili uendelee kupata msaada-ama sivyo msaada hakuna tena! Kufanya hivyo wanataka usizinduliwe kutoka usingizini na hao maadui zao.
5.       WATADHARAU/KUBEZA/KUYASHUSHA MAAMUZI/MAWAZO YAKO, Haijalishi Kama Yana Maslahi Kwako Katika Kukukomboa Na Utegemezi
Kama umezoea kwenda kuomba ushauri kwa mtu unayemtegemea sana akupe msaada, watu wenye kupenda uendeele kuwa mteja wa maamuzi yako watafanya kila hila kuhakikisha maamuzi au mikakati ya kuelekea kujinasua na utumwa/utegemezi inagonga mwamba. Watadharau na kukuona kuwa una mawazo mgando.
-->
Kufahamu jinsi ya kujikomboa na hali hii au utegemezi unaopelekea utumwa wa fikra na mtazamo: Tafuta na usome Kitabu-Mtazamo Wako Ni Upi? cha Mwandishi makini Henry Kazula.

Ikiwa unahitaji kujua zaidi SIRI 5 zilizobaki, tuma anwani ya barua pepe ukionyesha kuguswa na makala zetu kupitia jielimishekwanza@gmail.com, au tuma SMS yenye anwani yako kupitia 0754 572 143.Nasi bila hiyana tutakutumia makala hii yote, pia utakuwa wa kwanza kupata kila makala mpya kutoka Jielimishe Kwanza! Blog.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni