Picha na www.presstv.ir |
Kila
mwanadamu ameumbwa na hali ya kukumbuka na kusahau mambo mbali mbali
yanayomtokea kila siku.Katika hali zote kuna faida na hasara yake, tukiangalia
upande wa faida- mfano binadamu tunajihisi vizuri pale tunapokumbuka mambo
mazuri yenye kufurahisha yaliyowahi kututokea pia tunasahau mabaya, huzuni na
mengine yaliyowahi kutuudhi.
Tukirudi
katika mfumo wa kujifunza hakuna mtu atakataa kuwa angependa akumbuke mambo yote
aliyofundishwa na kujisomea ili afaulu mitihani na kupata cheti kizuri ilihali
utendaji na utumiaji wa hayo anayojifunza katika uhalisia ni hafifu.
Picha na www.upbeatlearning.com |
Wanafunzi
wengi wanapata shida na kukata tamaa ya kujifunza kutokana na aduni huyu mkubwa
aitwaye KUSAHAU.
Mtazamo wa Wanasaikolojia kuhusu
chanzo cha kusahau ovyo.
Tunawezaje kuboresha kumbu kumbu zetu na kuepukana na
tatizo la kusahau kwa kulinganisha unachokifahamu na unachotaka kukifahamu?
Ikiwa wewe ni mwanafunzi, jaribu kujihoji kwanza
ninafahamu nini? kabla ya kujifunza kitu kipya, husianisha kwa pamoja
ukizingatia kufanana kwa hizo taarifa au mambo hayo mawili.
Pia jaribu kuhusianisha maarifa unayojifunza na hali
halisi au vitu halisi.Ukitaka kukumbuka, hasa siku ya mtihani ni rahisi sana
kukumbuka vile vitu au maarifa tuliyokuwa tunayafahamu kabla…hivyo husianisha!
Utaona maajabu yake…hakika utakumbuka!
Ukitaka ufafanuzi au kujifunza zaidi kuhusu mbinu hii ya kuepukana na kusahau, tuwasiliane...
Imetolewa na
Jielimishe kwanza!