FURAHIA SIKU HII KWA KUDUMISHA URAFIKI IMARA!
Huu ni muendelezo wa makala ya jumanne tarehe 30 Julai 2013-http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/urafiki-siku-ya-kimataifa-ya-urafiki.html?utm_source=BP_recent
Leo ni siku kubwa duniani inayojumuisha
marafiki-wanaotaka kuboresha urafiki, pia wale wanaotaka kuanzisha urafiki
mpya.
Picha za www.unmultimedia.org |
Sanjali na siku hii yenye kuboresha mahusiano mema kwa jamii
mbali mbali za watu duniani…amani inaombwa itawale…sidhani kama una urafiki
ulio imara utawaza kumuua au kumwibia rafiki yako!
Tukiwa na malengo makubwa yenye kujenga au kuimaisha
urafiki, naomba nikupe muendelezo wa mambo 10 mengine muhimu ya kufanya kufikia lengo:
11.KUWA MUWAZI HASA UKIONGEA KWA HOJA
12.KUWA MTU WA KUKUBALI HASA KWA NJIA ZINAZOELEWEKA
13.JITAHIDI KUENDANA NA MABADILIKO
14.PATIKANA…TENGENEZA RATIBA KUKUTANA AU KUONGEA NA MARAFIKI
15.KUWA MSIKILIZAJI
16.KUWA MTU WA FURAHA
17.SAMEHE INAPOBIDI NA KUSAHAU
18.DHIBITI HASIRA YAKO…KABLA YA KUTOA MAAMUZI UKIWA NA
HASIRA, HESABU 1 HADI 100...itakusaidia kutoa maamuzi sahihi.
19.TUMIA BUSARA…MFANYE ADUI WA RAFIKI YAKO KUWA RAFIKI
20.TUNZA SIRI YA RAFIKI YAKO
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!