Picha na endoftheamericandream.com |
Hivi umewahi kujiuliza kwa nini matajiri
wanaendelea kuwa matajiri wakati huo huo masikini wanaendelea kuwa
masikini?
Tofauti kati ya makundi haya mawili ni kwamba,
matajiri wanawekeza zaidi kwa kutumia
pesa zao wakati huo huo masikini wanatumia
ovyo kwa kile wanachokipata.
Nikilinganisha hali hii kihistoria, hasa maisha
ya zamani ya babu na bibi zetu kutegemea uwindaji, ilikuwa ni hali iliyozoeleka
kwa wanaume kuaga familia zao asubuhi na mapema kwenda kutafuta kitoweo.Hii
ilikuwa ni hali ya kila siku ili kuweza kukidhi haja ya siku husika.
Kwa jamii za wale waliogundua siri ya kujilimbikizia mali waliamua kutengeneza boma la kuhifadhia wanyama
waliowategemea kwa mlo…hapa ufugaji ukaanza, kwa lengo la kujiepusha na
usumbufu wa kwenda kuwinda mara kwa mara pia uhaba wa wanyama kwa msimu fulani.Baada ya muda fulani wanyama
waliowafuga walizaliana na hatimaye kukidhi hitaji la kitoweo pia kuuza kwa
wengine wasiokuwa na maono ya kujilimbikizia kwa ajili ya baadaye.
Historia inatufundisha kujiwekea akiba ya
baadaye na si kuangalia maisha ya leo.
Kuna hatua mbili (2) muhimu wanazotumia watu
wenye mali nyingi na kuendelea kuwa jinsi walivyo:
1.KUWA NA MAAMUZI SAHIHI YA KUTUMIA PESA
KATIKA NJIA SAHIHI... mfano kununua kitu kwa kusudi maalumu na si kwa sababu imetokea tu au kwa sababu mtu mwingine anacho au tu kwa mashindano..la hasha!
2.KUJENGA “BOMA”
Kama nilivyotoa mfano wa kihistoria kuhusu
maisha ya watu wenye mali waliowahi kuishi, kwa maisha ya leo kuna mifumo mbali
mbali ya kuwa na boma nayo ni;
· KUJENGA BIASHARA
· KUTUNZA PESA (AU KUTUNZA VITU VINAVYOWEZA
KUTHAMANISHWA NA PESA WAKATI PESA IKIHITAJIKA)
· KUJIHUSISHA NA KUNUNUA VIWANJA, NYUMBA NA
KUKODIAHA/KUPANGISHA AU KUUZA KWA FAIDA
· KUWEKEZA KWENYE SOKO LA HISA
Makala hii imeandaliwa na Jielimishe Kwanza! kwa kushirikiana
na kitabu alichoandika mjasiriamali maarufu nchini Marekani Robert Kiyosaki-“Be Rich & Happy” Sura ya 19 ukurasa wa 195.
Ikiwa unahitaji
kitabu hicho tuwasiliane kupitia 0754 572 143.Ikiwa unaona uvivu kusoma
kitabu, fuatilia mbinu za kuanza kusoma kitabu kwa mafanikio kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/elimu-na-mtazamo-mbinu-10-za-kuanza.html
Usipuuze ushauri huu, kumbuka maneno ya tajiri mkubwa -Henry Ford, mwanzilishi wa kampuni ya magari aina ya Ford alisema;
"PAYING ATTENTION TO SIMPLE LITTLE THINGS THAT MOST MEN NEGLECT MAKES A FEW MEN RICH " -Henry Ford