Katika kuadhimisha sherehe ya kutumiza mwaka
1 siku ya Jumapili 25 Agosti 2013 kikundi hicho kijulikanacho kwa jina la “LUGALO GRADUATES’ NETWORK ASSOCIATION
-2001” kilichoundwa na vijana waliosoma Shule ya sekondari Lugalo Iringa- Tanzania kilionelea ni vyema kuwajibika katika
kutoa mchango kwa jamii ikiwa ni sehemu mojawapo ya malengo ya kikundi.
Kikundi hicho chenye wanachama hai 18 chini
ya uongozi wa Mwenyekiti-
Henry
Kazula kiliweza kutimiza adhma hiyo kwa kuwatembelea na kutoa msaada wa
vifaa vya matumizi ya kawaida vyenye thamani (shilingi laki moja) sh.100,000 kwa watoto yatima wa kituo
kiijulikanacho kwa jina la CHAKUWAMA kilichopo Sinza-Meeda jijini Dar es
salaam.
Wakiongea na Jielimishe Kwanza! wanakikundi hao
walieleza kuwa lengo kuu la msaada huo ni kushiriki kwa pamoja na kikamilifu kwa
mali na hali katika shughuli za kijamii kwa kile wanachokikusanya kutokana na
michango yao ya kila mwezi.
Pia walisema wamefanya hivyo kuweza kutoa
changamoto kwa wanajamii wengine kujitoa kwa hali na mali kusaidia watoto
yatima na si kusubiri hadi watu watoke nje ya nchi kutoa misaada.
Hii ni kutokana na matatizo kadha wa kadha
ndani ya vituo vya kulea watoto yatima ikiwa ni huduma mbovu za afya,ufinyu wa
malazi na ukosefu wa wataalamu wa kuwafundisha watoto hao malezi bora na stadi
za maisha.
Wakiungana kwa pamoja na Jielimishe Kwanza!
wanatoa rai kwa jamii kulivalia suala hili njuga ili kuijenga jamii ijayo yenye
maadili na tija kwa Taifa.
Walitoa angalizo kuwa kutowajali na kuwapuuza
watoto na vijana waishio katika mazingira magumu kunaandaa jamii/kundi hatari
sana kwa Taifa hapo baadaye.
Wasiliana na kikundi hicho kupitia 0785 175
157 au andika kupitia jielimishekwanza@gmail.com
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!