Picha na http://madonnarobinson.com |
Bila shaka umewahi kusikia vijana wengi
wakisema hivi “umri bado unaruhusu” au “mimi bado mdogo” kuhusiana na suala
zima la maisha ya kujitegemea na hata uthubutu wa kuelekea kwenye uwekezaji pia
kuwa na mali.
Nikilinganisha mtazamo huo na misemo ya
Kiswahili kama “Chelewa chelewa utakuta
mwana si wako” na “ujana maji ya
moto” yenye mantiki ya kuchukua hatua mapema bila kujali hali ya umri
ulionao au maisha yaliyopo naona kuna haja ya kubadilisha mtazamo.
Sanjali na hilo pia kuna msemo huu wa
Kiingereza uliozoeleka sana midomoni mwa watu- “Life is not a rehearsal, is a performance” ni ukweli usiopingika
kuwa tunatakiwa kuonyesha kiuhalisia jinsi tunavyoishi na si kujaribu au
kuigiza.Natumaini umejua namaanisha nini?
Hivyo basi tunatakiwa kuchukua hatua ya uthubutu wenye
tija-SOMA HII http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/vijana-na-maisha.html
ili kujinasua hapo tulipo na si kunung'unika huku tukisubiri tuzeeke na kutumainia malipo ya
uzeeni…wakati wa kuwekeza ni sasa kwa sababu tuna nguvu, ari na akili inafanya
kazi kwa haraka.
Fanya mabadiliko sasa kupunguza tatizo la utegemezi ndani ya familia na jamii kwa ujumla.
Vijana Taifa la Leo na Kesho!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!