-->
Jumamosi-Agosti 17, 2013 ilikuwa ni kilele
cha siku ya kutunuku tuzo kwa vijana kama ilivyokuwa imepangwa na “Youth for Africa (YOA)” ikishirikiana na
wadhamini mbali mbali.Soma undani wa maandalizi hadi kuifikia siku hii kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/zoezi-la-kutunuku-tuzo-kwa-vijana-chini.html
Ilikuwa ni siku nzuri iliyogubikwa na shamra
shamra, burudani zenye kuhamasisha vijana wengine na jamii kwa ujumla kuhusu kutumia
vipaji na uwezo binafsi kuwa na uthubutu kugusa maisha ya wengine.Ikiwa ni
sanjari na kauli mbiu ya YOA –“Born talented living to do it.” Naweza
kuongezea kwa kusema…and
influence other talented to do it!
Mgeni rasmi wa tukio hilo Mhe. Januari
Makamba(MB) aliwaamasisha vijana kuhusu kusoma vitabu ili kujiongezea uwezo na kuboresha mtazamo wa
kufikiri na kubuni mbinu mbali mbali kupambana na changamoto za maisha.Kwa kuzingatia umuhimu wa kusoma vitabu, Jielimishe Kwanza! imeliona hilo mapema na kutoa njia mbali mbali za kufanikisha kujisomea.Ukitaka
kujua umuhimu na siri iliyopo ndani ya vitabu soma hii: http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/ifahamu-siri-iliyopo-ndani-ya-vitabu.html?spref=bl na pia jinsi ya kuanza kusoma kitabu kwa mafanikio soma hii http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/elimu-na-mtazamo-mbinu-10-za-kuanza.html.
Naomba kutoa rai kwa wazazi kuanza kuwajengea uwezo watoto wao kujisomea vitabu...soma hii zaidihttp://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/elimu-na-malezi-mjengee-mtoto-wako.html
Pia Mhe.Januari Makamba(MB) alitoa pongezi kwa Asasi isiyo ya kiserikali -YOA http://www.yoa.or.tz/ ikishirikiana na wadhamini mbali mbali kwa kutambua uwepo wa vipaji na kuandaa tukio hilo kubwa.
Tuzo hizo zitakuwa zikitolewa kila mwaka kwa
kuzingatia maboresho zaidi ili ziwe na tija zaidi hasa kuwahamasisha vijana wa
Kitanzania na Afrika kwa ujumla kubadili mtazamo wa kufikiri kwa kuijenga
Afrika huru.
MATUKIO KATIKA PICHA:
Timu nzima ya YOA wakiwa na Mhe.Januari Makamba (MB). |