W
|
abunifu wa simu za mkononi wamekuwa wajanja
sana kwa kucheza na fikra na mtazamo wa watumiaji. Ukiangalia kwa makini lengo
la simu hizo linabaki pale pale-KUWASILIANA! haijalishi ni simu ya aina
gani-iwe ya gharama kubwa au ndogo.
Katika kipindi kifupi wabunifu hao wamefanikiwa kuteka fikra za watumiaji wengi duniani kwa kuongezea vikolombwezo
mbali mbali vya matumizi kama vile “Internet”,
mfumo wa kutumia ujumbe wa moja kwa moja kama Whatsup! Na mengineyo yanayowapendezesha watumiaji kama kioo cha
kugusa (kubonyeza ni shida!) na muonekano mzima wa simu.
Maboresho hayo ya simu kulingana na mitindo
ya yote niliyotaja hujumuisha ongezeko la gharama -( mfano kuna simu inayofikia hadi
Shilingi milioni mbili za Kitanzania).
Kulingana na mvuto wa simu hizo, makundi yote
ya watu kiuchumi yamekuwa yakivutika kwa kasi kununua simu hizo za gharama
kubwa.Yaani kwa lugha nyingine watu wameamua kufanya uwekezaji katika simu zao
za mkononi.Bila kujua, watu wamesahau lile lengo la msingi la simu za mkononi
la KUWASILIANA!
Ni kawaida kabisa kumuona mtumiaji wa simu,
akimiliki simu zaidi ya moja zenye gharama kubwa…wakati huo huo maisha yake
yakiwa duni.
Taarifa za hivi karibuni kutoka nchini
Denmark na nchi nyingine za Ulaya zimethibitisha kuwa watu wamekumbwa na msongo
wa mawazo kutokana na simu zao za mkononi “smartphone”
(hasa kutumia muda mrefu kuperuzi kupitia mitandao ya kijamii -facebook, twitter
n.k) pia kutokana na wimbi kubwa la mabadiliko ya teknolojia sanjali na simu za mkononi “smartphone” wakati huo huo wakitakiwa kufanya kazi na kuwasiliana na watu wanaowapigia simu. Kwa sasa baadhi ya watumiaji wengine wa simu hizo wameanza kurudia tena kutumia
simu zenye matumizi rahisi.
Pia soma hii http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/jamii-na-mawasiliano.html uone simu za mkononi zilipotufikisha.
Ushauri wa bure:
Ni vyema kuchukua hatua ya kujiuliza maswali haya ya msingi kabla ya kuwa na wazo la kununua simu mpya;
Ni vyema kuchukua hatua ya kujiuliza maswali haya ya msingi kabla ya kuwa na wazo la kununua simu mpya;
- Nanunua simu hii ili na mimi nionekane ninazo ilihali sina pesa?
- Nawekeza kiasi gani cha pesa kwenye simu yangu? Je, simu hii itakuwa inarudisha faida au itakuwa rasilimali isiyozalisha na yenye kutoa pesa mfukoni mwangu mara kwa mara?
- Simu ninayonunua itanisaidia kwenye masuala ya kazi na biashara kwa kuongeza ufanisi na kipato?
Huu ndiyo uhalisia, ni mtazamo tu! Tuangalie
sana, tunapaswa kuwekeza kwenye mipango endelevu ya maendeleo na si kwenye mitindo ya simu inayoingia kila kukicha. Lakini siyo mbaya kama unawekeza kwenye simu yako
bila kusahau maendeleo endelevu ya kijamii.
Soma hii http://www.medscape.com/viewarticle/804666 pia kujua zaidi kuhusu matumizi ya "Smartphone".
Soma hii http://www.medscape.com/viewarticle/804666 pia kujua zaidi kuhusu matumizi ya "Smartphone".
Imetolewa na
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni