I
|
Asasi isiyo ya kiserikali ijulikanayo kwa jina “Human Talent Watch" (H.T.W) iliyopo
Mbezi-Msuguli- jijini Dar es salaam imeanzisha program maalumu ya kuibua na
kukuza vipaji kwa vijana ijulikanayo kwa jina la “Evening Talk Program” ikimaanisha “maongezi rasmi ya jioni “ kwa
kuwashirikisha watu waliofanikiwa kwa kutumia vipaji ili kuwatia moyo na
kuwapatia mbinu vijana chipukizi katika
vipaji husika.
Programu hiyo maalumu na
yenye tija kwa vijana wenye vipaji nchini Tanzania ilizinduliwa Jumamosi , 9
Novemba 2013 na Mkurugenzi mtendaji wa Jielimishe Kwanza! ndugu Henry Kazula
majira ya jioni.
Akiongea moja kwa moja na
mwandishi wa Jielimishe Kwanza! mwenyekiti wa H.T.W ndugu Frank Mihayo alifanunua zaidi
malengo ya “Evening Talk Program”,
alisema;
…programu hii ni maalumu kwa kuwakutanisha vijana wenye umri kuanzia
miaka 12-35 pamoja ili kujifunza/kupata mbinu mbali mbali zitakazowasaidia
kutimiza ndoto zao. ”Evening Talk” ni chimbuko la la maarifa sahihi kwa
vijana-“a source of perfect knowledge”.Pia ni fursa maalumu kwa vijana
chipukizi wenye vipaji kukutanishwa na vijana mashuhuri waliofikia mafanikio ya
ndoto zao katika nyanja mbali mbali-sanaa,uchumi,uongozi na biashara.
Ndugu Mihayo alikazia zaidi kuwa, watu waliofanikiwa kwa vipaji vyao watapata
fursa ya kutoa mada zenye kuchochea hamasa ya mafanikio kwa vijana kupitia
vipaji. Kwa vijana chipukizi watapata fursa ya kujijengea hali ya
kujitambua,kujiamini,kujifunza mambo mapya kuhusiana na vipaji na kupata nafasi
kuunganishwa na wadau mbali mbali.
Katika kutimiza azma ya mpango huu kuna changamoto zifuatazo;
- Kukosa ukumbi wa kuendeshea programu hii
- Ukosefu wa fedha za uendeshaji kama kalamu na madaftari ya kuhifadhia kumbukumbu
- Fedha ya kuitangaza programu hii kwenye vyombo vingine vya habari ili vijana wengi wapate fursa ya kushiriki na kujifunza.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mkurugenzi mtendaji wa Jielimishe Kwanza! ndugu Henry Kazula akiongea na vijana wenye |
vipaji vya mpira,muziki na uigizaji.
Katika nyuso za furaha vijana wenye vipaji vya muziki,uigizaji na mpira wakiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Jielimishe Kwanza! ndugu Henry Kazula kwa pamoja na Mwenyekiti wa H.T.W ndugu Frank Mihayo. |
Mwisho wa yote, mgeni rasmi
alipewa fursa ya kuongea na vijana; alijaribu kuwashirikisha kwa kurejea moja
ya makala zake kupitia Jielimishe Kwanza! ijulikanayo kwa kichwa
“Jinsi ya kupaza sauti ya
mafanikio na jamii ikukubali" Soma hii http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/05/jinsi-ya-kupaza-sauti-ya-mafanikio.html
Ikiwa umeguswa na program hii
na unataka kuchangia kwa njia moja au nyingine usisitize kuwasiliana na
Mwenyekiti wa H.T.W kwa namba +255 752 297 264 au muandikie kupitia barua pepe humantalentwatch@gmail.com
Imetayarishwa, Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni