Na David Serikali,
MwanaTYVA na
Mwanafunzi wa Azania Sekondari.
W
|
akati pakiwa na
taarifa zinazosambaa kwa kasi kuhusu wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kudai
kuwa fedha wanayolipwa kwa siku ya kiasi cha shillingi laki tatu (300,000=/)
haitoshi hivyo waongezewe posho.
Nilipata muda na
kurejea kusoma kijitabu kidogo cha TUJISAHIHISHE kilichoandikwa na Raisi wa
TANU Julius K.Nyerere ili nirejee makosa yaliyofanyika kipindi cha TANU hadi
akaamua kuandika kitabu hicho.Ulikuwa ni wakati mzuri wa kugundua kuwa makosa
mengi hayajasahihishwa na yanaendelea, na yametufikisha hapa tulipo.Soma hii pia ili kujisahihisha makosa yetu.
J.K.Nyerere
anaandika anasema "Ukiondoa matatizo
yanayowapata binadamu kwa sababu ya mambo kama mafuriko,nzige,kiangazi na kadhalika
MATATIZO YAO MENGI HUTOKANA NA UNAFSI" jambo linalowafanya kuuliza
hali yao ya baadae itakuwaje na hufanya hivyo si kwa maslahi ya jamii ya
watu,bali kwa maslahi yao binafsi.
Hayo yameanza
kujitokaza ikiwa ni siku chache tu tangu wajumbe wa bunge maalum la Katiba
kuwasili huko bungeni kutimiza yale jamii iliyowateuwa na kuwaamini kuwa wanaweza fanya kazi waliyotumwa
na wananchi.
Hayati J.K.Nyerere
hakuishia upande mmoja tu,bali aliangalia upande wa pili wa shillingi na
kuandika akisema "Kosa jingine
linalotokana na unafsi tunalifanya wakati wa kuchagua viongozi,mahala pengine
viongozi ( na hata wawakilishi) wetu hawana budi watokane na WATU bila hila au
ujanja wa aina yoyote".Nimenukuu kifungu hiki nikihusisha na uhalisia
kuwa tayari kuna taarifa za ndani toka bunge hilo maalum la Katiba na pengine
katika vyombo mbalimbali ya habari kuwa kuna wawakilishi hawajaenda kuiwakilisha
jamii yao,bali ni kwa manufaa yao binafsi.
J.K. Nyerere anaendelea
na kusema "lakini mara nyingi
wawakilishwaji huchagua wawakilishi bila kufikiri kwa makini kuwa viongozi hao
wanaweza, au hawawezi kazi wanayochaguliwa kufanya.Wawakilishwaji watafanya
makosa makubwa saana kama watachagua viongozi wao ovyo tu. Kimsingi yote ni makosa na kosa la kwanza ni
tofauti na kosa la pili japo yote hutokana na Unafsi.”Swali la kujiuliza ni
kwamba"
Wakati pakiwa na
muendelezo wa matukio kadhaa kama haya, tunajifunza nini? na twapaswa
kujisahihisha wapi? Kama Mtanzania mwenye kulichukulia kwa uzito wa hali ya juu
Bunge maalum la Katiba nikijua fika ndipo mahali pekee patakapojenga hatma ya
Tanzania njema,bora na yenye matumaini kwa Watanzania wote leo kesho,kesho
kutwa au hata baada ya miaka hamsini ijayo tena,Wawakilishi wangeweka tofauti
zao za kimaslahi pembeni kwanza na kutafakari kukubaliana kutimiza kwa moyo wa
dhati majukumu watakayofanya wakiwa Bungeni-Dodoma kwa hizo siku na pengine
zaidi kadri ya ufanishikishaji wa Katiba hiyo mpya, tarajiwa ya Jamhuri wa
Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo napenda
kumalizia kwa kusema kadhaliwa matakwa na mapendekezo ya wachache pia
hujulikana katika mijadala,majadiliano na mazungumzo.Bila wachache kusema
waziwazi matakwa yao,mijadala na majadiliano hayana maana.Kwa kadri ya
mapendekezo na matakwa yao hao wachache waje na hoja na kupewa nafasi ya
kusikilizwa kisha wenye kupinga nao wapinge kwa hoja.
Hivyo ni matumaini
yangu kuwa wachache waliokuja na hoja ya kutokutosha kwa posho wanayolipwa,
hivyo kutaka kuongezewa… watakuwa na hoja kwanini waona hivyo? na wachache
wanaosema inatosha na kwa maana hiyo hapana uhitaji wa kuongeza posho hizo
watakuwa na hoja kwanini wao wanaona hivyo.Hoja hujibiwa kwa hoja.
Mungu ibariki
Tanzania.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni