Ndugu msomaji natumaini u
buheri wa afya na yawezekana unaendelea kufuatilia habari kem kem ili hali uwe
jirani na dunia.Sambamba na hilo naomba nikukumbushe kidogo kuhusu makala yetu
ya siku chache zilizopita kuhusu “je unajuaje kama kila unachoambiwa ni kweli?” ukizingatia kuwa tunapenda kupata habari mpya
kila siku.Tuliona kuwa ni vyema kuchunguza kwa kina na kujielimisha zaidi kwa
kusoma vitabu, makala, majarida mbali mbali na pia kusikiliza hotuba mbali
mbali ili kuboresha upeo wetu katika
kupambanua mambo, mwisho wa siku kuweza kujua ukweli wa mambo.Kinyume na hapo
tutakuwa ni watu wa kudanganywa tu, mwisho kuchukua maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati
husika!
Picha;http://www.tmf.or.tz/ |
Leo nataka nikulete kwenye
mandhali hiyo hiyo lakini nikijikita zaidi katika taarifa lukuki tuonazo na
kusikia kupitia vyombo mbali mbali vya habari vinavyojulikana na kuheshimika
kisheria.
Ama kwa hakika tumekuwa
mstari wa mbele kufuatilia kwa makini na kutaka kujua zaidi undani masuala
mbali mbali yanayojili na yaliyojili ndani na nje ya nchi kupitia vyanzo hivyo vya habari.Inafika wakati tunabaki njia
panda, hasa kwa kupata habari zilizo na mkakanganyiko na uzushi. Wakati
mwingine tunagundua kuwa vyanzo vingine vya habari hutoa na kupambisha habari ili viuze au kuboresha umaarufu wa watu fulani.
Wengi waweza kukubaiana nami
kuwa kuna wakati habari tunazosoma kupitia magazeti na majarida…(sina haja ya
kuyataja) huweka"headlines" / vichwa vya habari vya kuvutia sana lakini undani wa habari hukinzana kabisaaaa!!!! na hali halisi na matarajio ya
msomaji.
Pia kwa upande wa
televisheni zetu, ndugu msomaji unaweza kuwa shahidi; kuna mazingira ya habari
na matukio yanayoonyeshwa wakati mwingine kwa maslahi ya watu fulani ili
kujiimarisha kisiasa na kiuchumi na hata kutaka kuwa maarufu.Lakini ukizingatia
na kufanya utafiti wa kutosha utaujua
ukweli wa mambo kwa KUJIELIMISHA.
Ndugu msomaji, sina hakika
sana kuwa ni mara ngapi umewahi kujiuliza swali hili ambalo leo nauliza; “nini hasa hukuhamasisha kuwa habari kutoka
chombo fulani cha habari ukipendacho ni kweli?
Katika kutoa msaada wa
kuweza kujibu swali hili ni vyema ukasoma tena makala yetu kuhusu “ je unajuaje kama kila unachoambiwa ni
kweli?” utaona mbinu ya kuweza kuchuja habari tupokeazo kwa kusikiliza, kutazama na
kusoma.Ila, mbinu kubwa kuliko zote ni ile ya kufuatilia habari husika
ukilinganisha na vyombo vingine vya habari visivyopungua kumi…je vyanzo vyote vya habari husika vinasimamia
habari hiyo hiyo kama ilivyo? Hapa namaanisha tusichukulie uzito wa habari
katika chombo kimoja cha habari, hata kama ni chaguo lako…linganisha habari kwa
kuunganisha matukio…kwa msemo maarufu wa lugha ya Malkia wanasema “connecting dots”
Kuwa na mashaka sana kuhusu
habari iliyojenga “headline” ...vijana wa mjini hupendelea kuiita “habari
ya mjini” kupitia chombo kimoja tu cha habari! Wakati mwingine huwa ni
uzushi tu au chombo hicho cha bahari kutaka kumchafua mtu au kikundi cha watu
fulani, au kuuza habari…Ichunguze habari hiyo kwa makini sana, Jielimishe Kwanza! ili ufahamu
ukweli halisi wa mambo.
Nakutakia usomaji, utazamaji na usikivu
mwema wa habari ukijiridhisha kuwepo kwa ukweli ndani yake.
Makala hii imetolewa na
Jielimishe Kwanza! Social Enterprise kwa udhamini wa Ide@Spot na Enviro-Forum.
Habari /maulizo:jielimishekwanza@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni