Bila shaka tumefuatana vizuri katika makala zetu kwa kuzingatia dhana nzima ya kutambua viashiria vya utumwa
wa kisasa-“Modern Day Slavery” na
athari zake kwa mfanyakazi awaye yote katika kada mbali mbali za ajira.
Utumwa huu kama ilivyoanishwa awali upo
kwa kificho sana na umeota mizizi. Wafanyakazi wengi huchukulia hali hiyo kuwa ni sehemu ya
kawaida ya kutimiza majukumu ya kazi kwa lengo mahsusi la kujipatia kipato.
Baadhi ya wafanyakazi nchini Tanzania na
kungineko duniani hufikia hatua ya kulalamikia mamlaka husika kwa maandamano ya
hisani bila matumaini na wakati mwingine inafikia hatua ya kutishiwa kuachishwa
kazi.
Sasa imefika wakati wa wafanyakazi na
wanajamii kwa ujumla wake kuungana kwa pamoja bila kuwa na hofu ili kutokomeza
chembe chembe zozote za “utumwa wa
kisasa” katika maeneo yasiyo rasmi na rasmi ya kazi.
Licha ya kuungana, mfanyakazi anaweza
kufanya yafuatayo ili kutokomeza “utumwa
wa kisasa” bila mwajiri wake kujua (itambulike
kuwa waajiri huitaji ubora wa kazi na uzalishaji wenye tija kutoka kwa
mfanyakazi) na kuendelea kuwa mfanyakazi bora mwenye kipato cha kutakata.
Itaendelea...
Imetayarishwa na Jielimishe Kwanza! Social enterprise
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni