Kama tulivyoona wiki iliyopita
kuwa kuna madhara makubwa ya kumweleza mtu mwingine SIRI yako uionayo kuwa ni nzito, kubwa zaidi likiwa ni lile la kupoteza
uhuru wako.
Katika hali nyingine isiyo
ya kawaida, wapo watu wengine hujisikia vizuri na huru zaidi wakielezea SIRI
zao kwa wengine (wanajihisi kama wametua
mzigo wa kitu fulani kutoka moyoni) lakini wakati huo huo hujitahidi kwa
hali na mali kuilinda SIRI waliyoitoa isivuje.
Tuungane tena leo, ikiwa wewe
huwezi kujizuia kutunza SIRI yako mwenyewe…yaani unaona kama inakuwasha na hivyo
kuchukua hatua ya kumwambia mtu mwingine; fanya yafuatayo kujikinga na kupoteza uhuru wako wakati unapotaka
kutoa SIRI yako kwa mtu mwingine:
1.Ifanye
SIRI yako kuwa ya kawaida, ielezee kawaida na usimwonyeshe mwingine kuwa
imeshikilia furaha ya maisha yako.
2.Angalia
au chagua kwa uangalifu mtu wa kumwelezea SIRI yako, asiwe kama wewe uliyeshindwa kuitunza SIRI hiyo (…natania tu!)
3.Chagua
wakati muafaka wa kueleza SIRI yako.Ikiwa umempata rafiki wa kumwelezea SIRI
yako, jitahidi kusoma mazingira ya huyo unayetaka kumshirikisha SIRI yako.
4.Usionyeshe
kutoa motisha ya aina yeyote ile kwa mtunza SIRI wako.Ikiwa mtunza SIRI wako
anakutishia kuwa usipompa kitu fulani; mambo
hadharani, mwonyeshe kuwa huna wasi wasi wowote.
Kuhusu SIRI, msemo huu wa Kiswahili
unatawala-
“Hakuna
SIRI ya watu wawili”.
Imetayarishwa na
Henry Kazula-Mwandishi wa kitabu-“Mtazamo Wako Ni Upi?”
Na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni