Kunguru mweusi-Corvus splendens(Picha nawww.tanzaniabirds.net) |
Kwa
kipindi kirefu kunguru weusi ambao Kibailojia hujulikana kwa jina Corvus splendens wamekuwa ni kero kwa
maisha ya binadamu ikiwa ni ndege wanaomtegemea binadamu kwa kula mabaki ya
vyakula vinavyotupwa ovyo,vifaranga vya kuku,bata na wanyama wengine wadogo
wafugwao na ndio maana hujulikana kwa jina la Kiingereza “Indian House Crow” asili yao kutoka nchi za Kusini-Mashariki ya Asia
katika nchi za China,Cambodia,Thailand,India na Sri-Lanka.
Kunguru weusi wana sifa zifuatazo: wana akili
sana kiasi kwamba wanatambua mitego na silaha za moto,wanashambulia kwa pamoja
wakiwa kwenye kundi, wana uwezo wa kuhakikisha kuwa wanapata vyanzo vya
chakula.
Sifa nyingine ni kama:hawamwogopi binadamu,
wanategemea makazi yao jirani na makazi ya binadamu,wanazaliana kwa kasi sehemu
yoyote yenye idadi kubwa ya watu, ni wakorofi,wenye kelele na ushindani wa hali
ya juu katika suala zima la kupata chakula.
(http://nitawriter.wordpress.com/2009/05/25/the-indian-house-crow-should-not-thrive/).
Ndege hawa waliletwa na Serikali ya
Uingereza katika visiwa vya Zanzibar mwaka 1890 kwa lengo la kusafisha Mji
mkongwe kutokana na ongezeko la uchafu.
Mnamo mwaka 1950-1955 kunguru weusi walifika
Pwani ya Dar -es -salaam kwa njia ya majahazi na meli na kusambaa katika mikoa
mingine kama vile Pwani,Lindi,Morogoro,Tanga na Mtwara.
Kutokana na kero kubwa kwa maisha ya
binadamu,Wizara ya maliasili na utalii nchini Tanzania imeazimia kuwangamiza
kunguru weusi kutokana na sababu zilizo sambamba na kero hizo;
·
Wanaeneza vimelea vya magonjwa mbali mbali kwa
binadamu na kuku ikiwa ni pamoja na homa ya matumbo(Typhoid),kipindupindu na
mdondo(Newcastle disease)
· Wamekuwa na madhara na tishio kubwa kiikolojia
kwa kuharibu viota,kula mayai na makinda ya ndege wengine wa asili na wanyama
jamii ya mijusi
·
Huaribu miundo mbinu kama vile nyaya za
umeme,simu na antenna za runinga
·
Kero kubwa kwa wakazi wa sehemu mbali mbali
ikiwa ni pamoja na tabia yao ya kudokoa vyakula
· Wamekuwa na tabia ya kutawanya uchafu
uliokusanywa mahala pamoja, hivyo kuchafua mazingira
Serikali ya Tanzania ikishirkiana na Balozi za
Denmark,Finland na USAID imeamua kuchukua juhudi za makusudi za kuwaangamiza
ndege hao kwa kutumia mitego na sumu aina ya DRC 1339.Utekelezaji wa mradi huu
ni wa miaka mitatu kuanzia Mwezi Novemba 2010 na kutarajiwa kukamilika Mwezi
Desemba 2013.
Huu ni mtego maalumu unatumika kuwanasa kunguru weusi pekee (Picha na www.elitenetzwerk.bayern.de ) |
Wizara ya Maliasili na Utalii inakumbana na
changamoto zifuatazo katika zoezi zima la kuwateketeza kunguru weusi:
·
Gharama kubwa kwa ajili ya kununulia sumu DRC
1339 ambayo kwa kilo moja ni dola za Kimarekani 2500.
·
Kukithiri kwa uchafu hasa katika madampo
yaliyowekwa kiholela mitaani ambayo ni chanzo kikuu cha chakula kwa kunguru
weusi
·
Kunguru weusi hujifunza vyanzo vya kifo kwa
haraka hasa pale wanapouawa kwa kutumia sumu na mizoga kutokusanywa mapema
·
Ni vigumu kupata idadi kamili ya kunguru weusi
wanaouawa kwa kutumia sumu.
·
Uharibifu wa mitego unaofanywa na wananchi
katika baadhi ya maeneo.
·
Kasi kubwa ya kusambaa kwa kunguru weusi hususan
katika miji ya Pwani ya Bahari ya Hindi.
Tukishirikiana kuhifadhi taka za mabaki ya vyakula katika vifaa
vilivyofunikwa vizuri na kutupa kwenye madampo yaliyo mbali na makazi inaweza
ikawa njia mojawapo ya kupunguza idadi yao.
Makala hii imeandikwa kwa Kushirikiana na
Kijarida cha Wizara ya Maliasili na Utalii-Tanzania kilichotolewa kwenye maonyesho ya
Biashara(Saba Saba) mwaka 2013 na tovuti ya http://nitawriter.wordpress.com/2009/05/25/the-indian-house-crow-should-not-thrive/.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni