inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumatano, 7 Januari 2015

MTAZAMO: RUDISHA FURAHA ILIYOPOTEA KWA KUFANYA YAFUATAYO…



________________________________________ 

Picha:http://www.hischerishedones.org
Furaha ni hali ya kibinadamu inayotawaliwa na hisia au akili, hujitokeza kiasilia kwa kuchangiwa na mazingira mazuri yanayomzunguka mtu katika shughuli zake za kila siku.Humfanya mtu kujisikia vizuri, kujihisi kutosheka. Pia, ni kichocheo cha kusonga mbele kiutendaji na kuboresha maisha.

Kila mtu anapenda au anahitaji kuwa na furaha wakati wote.Swali la msingi la kujiuliza; Je, inawezekana kuwa na furaha wakati wote? Kiuhalisia, mwanadamu ameumbwa kukutana na changamoto mbali mbali zichocheazo utashi wake au hisia zake.Uwezo wa asili na akili ya binadamu kupambana na kushinda changamoto hizo huongeza furaha.Lakini, si kila changamoto iliyopo na inayojitokeza hupelekea furaha…kuna wakati hali huwa kinyume na matarajio kiasi cha kupoteza furaha. 
Shughuli za binadamu na mwenendo wa maisha yetu huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuikaribisha au kuikimbiza furaha iliyo asili ya mwanadamu, ondolea mbali mambo tusioweza kuyazuia kama kifo, magonjwa, dhoruba mbali mbali n.k. Hivyo basi, si jambo rahisi kuwa na furaha wakati wote! Hii ni sawa sawa na kusema hatuwezi kuipata furaha ya milele tungali tunaishi katika dunia hii yenye kila aina ya udhalimu na maovu.
Ingawaje hatuwezi kuwa na furaha wakati wote, tumaini lipo na tunaweza kuirejesha furaha iliyopotea kutokana na mambo yaliyo katika uwezo wa kibinadamu hasa kutokana na maisha ya kila siku na shughuli mbali mbali za kila siku.
Je, umepoteza furaha kwa kufeli mtihani?, kukosa ajira?, kukimbiwa na marafiki?, kutengwa na ndugu?, kuachwa/kukimbiwa na akupendaye(mke/mume au mchumba?), kuchekwa na watu kwa jinsi ulivyo? na hali nyingine zinazofanana na hizo? Usikate tamaa wala kurudi nyuma.Chukua hatua hizi 10 za ujasiri au ushujaa kufanya yafuatayo; (leo zitaainishwa 5):


1.ACHA KUNUNG’UNIKA, CHUKUA HATUA YA KUANZA UPYA!
Jinsi unavyoendelea kunung’unika ni dhahili kuwa hali itaendelea kuwa jinsi ilivyo na ndivyo fursa nyingi zitakapokupita.Manung’uniko huchochea hasira na chuki hivyo kuzidi kuipoza furaha yako. Hivyo, ni vyema kuacha kunung’unika na kuchukua hatua ya ujasiri kuanza upya, anzia ulipo ukiboresha mapungufu yaliyopo.
2.USIGEUKE NYUMA/USIKUMBUKE YALIYOPITA, SONGA MBELE!
Hakuna kitu kibaya kama kuendelea kukumbuka maumivu au matukio mabaya yaliyopita! Shukrani kwa Mungu hata kutuumbia hali ya kusahau…katika hali hii, kusahau mabaya hutupatia mtazamo chanya wa kuyaona maisha katika sura iliyo rafiki na kutujengea furaha nyingine.Songa mbele, jiwekee mkakati wa kutokumbuka yaliyopita.Najua kuwa kuna matukio mengine ni vigumu kuyasahau-lakini jitahidi kujibidisha, kuna wakati utafika na kuiona furaha yako ikirejea.
3.TAMBUA KUWA, ULIVYOVIPOTEZA HUKUZALIWA NAVYO…
Ni jambo la kipekee sana kumshukuru Mungu kwa kuwa tunaishi! Vile tulivyo ni upekee tuliopewa.Tumezaliwa na kuvikuta vitu na watu mbali mbali.Pia tunategemeana katika masula mbali mbali katika kuendesha gurudumu la maisha.Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna kitu tumezaliwa nacho…vingi tumevikuta na tunavitafuta kila kukicha.Pia, vingine ni vigumu kuvirudisha katika hali ya mwanzo.Hivyo,tunavyovipoteza visitukatishe tamaa na kupoteza furaha zetu.Tunapaswa kuanza upya kuanzia pale tulipo kama ilivyoelezwa katika hatua mbili zilizopita.
4.USIJIONE KUWA NI WEWE PEKEE MWENYE SHIDA IPELEKEAYO KUKOSA FURAHA…
Hatua hii inanifanya nikukumbushe moja ya makala zetu yenye kichwa Tambua kuwa wengine pia wana shida zao”kwa mantiki kuwa hakuna mtu asiye na shida; tunatofautiana jinsi ya kuziona shida na kupambana nazo.Ikiwa umepatwa na maswahibu yapelekeayo kupoteza furaha yako, ni vyema kutafakari kuwa hauko peke yako…yawezekana wewe una unafuu mkubwa kuliko wengine wenye shida.
5.JIJENGEE MTAZAMO MPYA WA MAISHA ULIO CHANYA…
Katika kitabu “MTAZAMO WAKO NI UPI? Mtazamo Wako, MaishaYako” kinaeleza na kuhamasisha mtazamo ulio chanya kwa kuwa maisha yetu hutawaliwa kwa kiasi kikubwa na mtazamo tulio nao na tunaotaka kuwa nao.Jitahidi kujiepusha na hali au mazingira yenye kukatisha tamaa, hali ya majonzi na kusononeka nafsi (mtazamo hasi) ili kuijenga na kuiimarisha furaha iliyo asili yetu. 
Tukutane tena siku nyingine kama hii tumalizie hatua 5 zilizobaki.
Mwandishi wa Kitabu-Mtazamo Wako Ni Upi?
Ushauri zaidi +255 (0) 754 572 143
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni