Picha na seriouslymen.com |
Ifahamike kuwa binadamu haishi
kama kisiwa; anaishi kwa kutegemea, kutegemewa pia kwa kutegemeana na wengine,
pia viumbe hai na visivyo hai.Kusema hivi nakumbuka mwaka 2005-2009 nilipokuwa
nikifundisha somo la “Elimu ya Viumbe-Baiolojia”
katika mada ya Ikolojia ngazi ya
shule za sekondari kuwa; viumbe hai (mimea na wanyama) hutegemeana pia
hutegemea viumbe visivyo hai kama hewa, maji, ardhi n.k.Hii hupelekea kuwepo
kwa mlishano wenye kutegemeana ili kuishi na kuendeleza kizazi.Napenda
kukumbushia tu kuhusu kutegemeana!
Sihitaji kuingia ndani zaidi
ya hapo, sipendi kuigeuza safu hii darasa la Baiolojia. Moja kwa moja nianze na
safu hii kwa kumlenga binadamu nikidhamilia kurusha mkuki kwa watu wanaopenda
wengine wawategemee kupita kiasi ili wawafanye watumwa/mateka wa fikra na
hatimaye kupora uhuru wao.
Makala
inayohusiana:
Hivi ndivyo uhuru wako unavyoweza kutekwa
Ndugu msomaji, ikiwa
unahusika au huusiki kwa kuwafanya wengine wakutegemee kupita kiasi napenda nikujuze
SIRI 10 zilizojificha na zinayoonekana kuwa hali ya kawaida katika maisha ya
kila siku. Watu hao wanaoonekana au kujiona wajanja huwafanyia watu wengine yafuatayo
kwa kujua au kutokujua ili kuwaweka kwenye mtego wa kuwa watumwa wao kifikra,
kimtazamo, kiutendaji na waendelee kuwa tegemezi;
1.
HUWAPATIA WENGINE “Samaki Na Si Nyavu...”
Katika lugha rahisi ni kuwa
hawakupatii ujuzi au mbinu au msaada ujikomboe mwenyewe na shida ulizonazo.Hutumia
kanuni iliyoainishwa na mwandishi wa 48-Laws of Power
akisema; “Never teach them enough so that they can do without you”. Katika tafsiri ya Kiswahili
isiyo rasmi-Usiwafundishe vya kutosha ili
washindwe kufanya lolote bila ya wewe”
2.
HUTOA
MSAADA WA FEDHA KWA DHAMANA YA KITU KINGINE CHA THAMANI WANACHOONA WENGINE
(WATUMWA WAO) WANACHO
Ikiwa unapokea msaada wa
fedha kutoka kwa mtu wako wa karibu na kuwekewa sharti-nitakupatia fedha unazohitaji ukinipatia…...au “nakupatia hizi hela ila itabidi unipe……” ujue
unakaribia kuingia kwenye mdomo wa simba.
3.
HAWAELEZI SIRI YA
KUFANIKIWA KWAO
Watu au makundi ya watu wanaopenda uwategemee, hata
siku moja hawatoi siri ya kufanikiwa kwao…wataeleza mafanikio yao juu juu tu
katika lugha tamu iliyozoeleka na wengi kama kujituma na juhudi binafsi-hivyo watakuambia fanya kazi kwa bidii! Ni
vigumu kwao kutoa ile silaha ya kufanikiwa kwao kwa watu wanaowachukulia kuwa
watumwa au wategemezi wao.
4. WANAKUCHAGULIA MARAFIKI
Ikiwa wamekuweka mikononi mwao; yaani unawategemea
katika msaada, wataanza kukuchagulia marafiki wa kuambatana nao walio marafiki
kwao na kutaka ujitenge na maadui wao au waliowazidi mbinu za kiuchumi.Haijalishi
kama una urafiki wa karibu na hao maadui zao, itakulazimu tu ujitenge nao ili
uendelee kupata msaada-ama sivyo msaada hakuna tena! Kufanya hivyo wanataka
usizinduliwe kutoka usingizini na hao maadui zao.
5. WATADHARAU/KUBEZA/KUYASHUSHA MAAMUZI/MAWAZO YAKO, Haijalishi Kama Yana Maslahi Kwako Katika Kukukomboa Na Utegemezi
Kama umezoea kwenda kuomba ushauri kwa mtu
unayemtegemea sana akupe msaada, watu wenye kupenda uendeele kuwa mteja wa
maamuzi yako watafanya kila hila kuhakikisha maamuzi au mikakati ya kuelekea
kujinasua na utumwa/utegemezi inagonga mwamba. Watadharau na kukuona kuwa una
mawazo mgando.
Kufahamu jinsi ya kujikomboa na hali hii au utegemezi
unaopelekea utumwa wa fikra na mtazamo: Tafuta na usome Kitabu-Mtazamo Wako Ni Upi? cha Mwandishi makini Henry Kazula.
Ikiwa unahitaji kujua zaidi SIRI 5 zilizobaki, tuma
anwani ya barua pepe ukionyesha kuguswa na makala zetu kupitia jielimishekwanza@gmail.com, au tuma SMS yenye anwani yako kupitia 0754 572 143.Nasi bila
hiyana tutakutumia makala hii yote, pia utakuwa wa kwanza kupata kila makala mpya kutoka Jielimishe Kwanza! Blog.