inspire
Lebo
business consultancy
Business consulting-2
Swahili translator
E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?
TANGAZO TUWEZESHANE
DUNIA IKUONE
Jumamosi, 29 Juni 2013
Ijumaa, 28 Juni 2013
MICHEZO:HISPANIA YAIONDOA ITALIA KWA "MATUTA" HAPO JANA...TAZAMA MATUTA YALIVYOKUWA!
BOFYA KIUNGANISHI UONE PENATI 14 "LIVE" KUPITIA:
JAMII NA MAWASILIANO: HIVI NDIVYO SIMU ZA MIKONONI ZINAVYOTUTENGA…
Mfumuko wa Teknolojia ya mawasiliano na
upatikanaji wa simu za viganjani kirahisi hasa zenye intaneti zimetufikisha
hapa tulipo. Si kwa lengo baya bali jema kabisa endapo tutakuwa na mipaka ya
matumizi na kuchagua vitu muhimu vya kuangalia tukizingatia kutunza wakati.
Tukiendekeza sana urafiki na simu ya mkononi
kwa kuchati…tutajikuta tupo mbali na eneo halisi tulipo.Hii ni hatari, kwa
sababu itamfanya mtu asijue kitu kinachoendelea jirani yake na wakati huo huo akiwa
makini na mambo ya mbali.
Mfano: mtu anakata mazungumzo na mtu aliye naye
jirani na kujikita na mawasiliano ya anga hivyo kushindwa kutimiza lengo la
kuwa jirani.
Hivi sasa, ndani ya familia kumekuwa na
migogoro mingi inayosababishwa na kuendekeza matumizi ya simu kupita
kiasi.Wazazi hawaongei na watoto kuhusu malezi na kumwachia mwalimu aitwae
“Teknolojia ya Habari na Mawasiliano-TEHAMA” afanye kazi yake.
Nikirejea makala yangu kuhusu umuhimu wa
TEHAMA kwa wanafunzi kujifunza ya Jumatano,19 Juni 2013-http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/elimu_19.html.Ni vizuri kumtumia
mwalimu huyu, lakini tujue fika kuwa anafundisha kila kitu; mema na mabaya kama
hakuna uangalizi wa kutosha na uelimishaji sahihi wa matumizi ya teknolojia
hii.
Kuthibitisha ukweli wa jambo hili, tazama video ifuatayo;
Kuthibitisha ukweli wa jambo hili, tazama video ifuatayo;
Hili ni angalizo tu, naomba nisieleweke
vibaya…hii ndiyo hali halisi inayoendelea siku hadi siku.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Alhamisi, 27 Juni 2013
HABARI MUHIMU: HIVI NDIVYO OBAMA ALIVYOINGIA NCHINI SENEGALI...
Ndege
waliyosafiria ijulikanayo kama “Air Force One” imegusa ardhi ya mji mkuu wa
Senegali-Dakar siku ya Jumatano jioni.Raisi Obama na familia yake wanatarajia
kuendelea na ziara yao nchini Afrika Kusini na Tanzania.
Karibu Tanzania!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Jumatano, 26 Juni 2013
MTAZAMO: JIFUNZE KUWA NA MTAZAMO CHANYA!
Picha na www.narconon.co |
Habari!
Naomba niwakaribishe tena katika ukumbi huu
kuhusu “MTAZAMO”.Wiki iliyopita niliandika makala kuhusu MADHARA YA KUWA NA MTAZAMO
HASI…
ISOME HAPA: http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/epuka-kuwa-na-mtazamohasi-picha-na.html
Mwishoni niliahidi kukuletea mbinu za kumfanya mtu kuwa na mtazamo chanya. Karibu tena leo kuzifahamu mbinu hizo.
Awali ya yote ni vyema tukafahamu faida za
kuwa na mtazamo chanya;
· Ni njia nzuri kiafya ya kuepukana na hatari ya
kupatawa na magonjwa ya moyo, pia huchochea kinga ya mwili
· kujiongezea uwezo wa kutatua matatizo
·
ni rahisi kwa watu wenye mtazamo chanya
kupambana na msongo wa mawazo
· mtazamo chanya huvuta vitu chanya-hii ni
sambamba na kufungua milango ya mafanikio katika maisha
· Katika hali ya muonekano wa kwanza, mtazamo
chanya utakufanya ukubalike na watu
Zifuatazo ni mbinu zinazoweza kumjengea mtu
uwezo wa kuwa na mtazamo chanya na wenye tija;
1.TUMIA LUGHA ILIYO CHANYA- USISEME “SIWEZI
KUPATA”…SEMA “NITAPATAJE?”…
Mjasiriamali maarufu na mwandishi wa vitabu
aliyebobea nchini Marekani-Robert Kiyosaki anatoa mtazamo huo katika hali ya
swali “NITAPATAJE?” akimaanisha kuwa swali hili litaubidisha ubongo kufikiri
njia mbadala za kupata suluhisho la tatizo.
Anapingana na usemi wa kwanza ulio
katika sentensi kamili “SIWEZI KUPATA” akimaanisha kuwa mtazamo huu hasi
unamfanya mtu kuwa mvivu wa kufikiri.
Anasisitiza kwa kusema kujiuliza maswali ni
njia moja wapo ya kuupa ubongo mazoezi na kuuongezea uwezo wa kufikiri, na
mwisho wa yote ni kupata mafanikio tarajiwa.
2.EPUKA KUELEZA MALENGO YAKO KWA KILA
MTU…UTAKATISHWA TAMAA!
Jifunze kuchagua mrafiki wa kuwaeleza malengo
yako…kuwa makini sana! Wapo wengine kazi yao ni kukukatisha tamaa.Ukitaka
kuwajua mtazamo wao, sikiliza maneno yao.
Angalizo: wapo watu watakaotaka kuboresha wazo/lengo lako kwa lugha ya kuonyesha ufanye marekebisho au maboresho, usiwabeze...chukulia hiyo kama changamoto kusonga mbele na kufanya vizuri zaidi.
3.JIFUNZE NA UFANYIE KAZI ULIYOJIFUNZA UKIWA
NA MTAZAMO CHANYA
Katika maisha ya kila siku tunajifunza kwa
njia moja au nyingine…jukumu letu ni kuchagua kujifunza mema au mabaya.Nikizungumizia
kuhusu kujifunza mema na yote yanayojenga ni vyema kuyafanyia kazi kwa vitendo
tukitegemea majibu chanya.Kadri utavyokuwa ukipima mafanikio ya utendaji ndivyo
unavyozidi kujiimarisha zaidi katika kuwa na mtazamo chanya.
4. JIWEKEE MALENGO KWA MAANDISHI
Ni kitu cha muhimu kuweka malengo-yanaweza
kuwa ya muda mfupi au mrefu.Mara nyingi malengo ya muda mfupi hutupa ari ya kuyakaribia malengo ya muda mrefu, pia ni sehemu ya kutuepusha kukata tamaa tukiwa katika safari ya kuelekea kwenye malengo ya muda mrefu.Kipimo cha mafanikio ya malengo yako kitaweza
kuboresha uwezo wako wa kuwa na mtazamo chanya.
5.JIHUSISHE NA WATU WENYE MATEGEMEO CHANYA
Kujihusisha na watu wenye mtazamo chanya
kutakuongezea uwezo wako wa mategemeo chanya katika mambo unayofanya.Pia
watakupa ari ya kusonga mbele kimawazo na kiutendaji.
6.FAHAMU FAIDA ZA KUWA NA MTAZAMO CHANYA
Ukifahamu faida za kuwa na mtazamo chanya
utajibidisha kufikia lengo la kuwa na mategemeo chanya.
7.JIWEKEE MPANGO WA KUEPUKA KUWA NA MTAZAMO
HASI
Panga utaratibu ulio kwa vitendo kuepukana na
mtazamo hasi.Kwa kufanya hivyo, mtazamo chanya utazidi kujijenga siku hadi siku.
8.TAMBUA NA UPAMBANE NA MAWAZO HASI
Kuna msemo unasema, kulijua tatizo ni njia
mojawapo ya kuoambana na tatizo au kumfahamu adui ni njia nzuri ya kuanza
kupambana naye.Jaribu kujichunguza utagundua ni kwa kiasi gani au mara ngapi
umekuwa na mtazamo hasi hata kwa vitu vilivyo kwenye uwezo wako?
9.JARIBU KUFANYA VITU VIPYA
Unapokuwa na uthubutu wa kutenda vitu vipya
ni njia ya kujiongezea ujasiri na kuimarisha mtazamo chanya wa kufikiri.Usiogope
kufanya makosa, hayo yanakuwa ni ishara ya kukuboreshea utendaji wako kwa kujifunza.
10.JISOMEE VITABU NA MAJARIDA
Kupitia vitabu na majarida utajifunza mambo
mengi kuhusu kujiimarisha katika mtazamo wa kufikiri hasa ukilinganisha na
wako.Ukitendea kazi mbinu mbali mbali zilizotolewa zitakuongezea uwezo wa kuwa
na mtazamo chanya siku hadi siku.
11.SIKILIZA HOTUBA NA MAFUNDISHO YENYE
KUIMARISHA
Kusikiza hotuba na mafundisho yenye
kuimarisha ukiwa kwenye gari au nyumbani ni njia nzuri kujiongezea uwezo wa
kuwa na mtazamo chanya.Kupitia hao utajifunza mbinu walizopitia kufikia malengo
yao.
Tuma maoni kupitia:jielimishekwanza@gmail.com
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Jumanne, 25 Juni 2013
NUKUU MAARUFU YA LEO: KUONDOKANA NA UMASIKINI...
Nelson Mandela(Picha na www.guardian.co.uk) |
"Kuondokana na umasikini si
suala la kutoa msaada wa pesa,ni suala la kutenda haki.Kama ilivyo kwa utumwa
na ubaguzi wa rangi,umasikini si wa asili.Unatengenezwa na mtu na unaweza
kuondoshwa kupitia matendo ya wanadamu."-NELSON MANDELA.
Jumapili, 23 Juni 2013
FAMILIA: UGOMVI WA WAZAZI… WATOTO KUKOSA MUELEKEO!
Malezi
bora ya watoto huchangiwa na ushirikiano wa pamoja wa baba na
mama.Kisaikolojia, mtoto hujengeka na kuwa na furaha kutokana na kuwepo kwa
furaha na upendo wa wazazi.
Ifahamike
kuwa muunganiko wa wazazi kwa ndoa au la unaimarika zaidi kwa kuwepo na
mtoto/watoto. Licha ya kuwepo na tofauti za hapa na pale ndani ya wapendanao
lakini haitakiwi watoto wajue tofauti zilizopo.
Picha imetolewa:www.ehow.com |
Ugomvi
wa aina yoyote ile unatakiwa kupata usuluhishi wa watu wawili(baba na mama)
kama walivyoanza wakiwa chumbani…watoto/mtoto hawapaswi kujua kinachoendelea
isipokuwa wawaone wazazi wakipendana na kuona furaha ikitawala ndani ya familia.
Hali
ikizidi kuwa mbaya, basi usuluhisi unaweza kufikishwa katika ngazi nyingine za
usuluhishi kama viongozi wa dini,wazee wa familia na ngazi nyingine zinazofaa.
Katika
jamii zetu tunazoishi, hasa kwa kipindi hiki kumekuwa na tabia iliyozoeleka kwa
wazazi kugombana mara kwa mara na kufikia hatua ya kutengana kwa sababu wanazojijua bila ya kujali kuwa wamezaa watoto.
Madhara ayapatayo mtoto kwa wazazi kugombana na kutengana
Hapa
nitatoa baadhi ya madhara yanayoonekana kirahisi ayapatayo mtoto/watoto kwa wazazi
kugombana na kutengana kwa talaka au njia nyingine;
- Mtoto anaweza kujengeka na tabia ya ugomvi-hii ni elimu ya awali kabisa kutoka kwa wazazi wake
- Suala la wazazi kutengana linaweza kuwafanya watoto kuwa njia panda-waende kwa mama au baba kwa sababu hawana chuki na wazazi wao(wanawapenda wote).Endapo wataenda na kukubaliana na mawazo ya mzazi mmoja, mwingine anakasirika na kusema watoto wa siku hizi wanadharau wazazi wao.
- Mtoto anaweza kuondoka nyumbani na kuamua kuishi maisha yake kwa sababu upendo umetoweka nyumbani.Hili humuweka mtoto kuwa huru kufanya lolote kwa sababu ushirikiano wa kumlea umevunjika.Pia ni kichocheo kikubwa cha ongezeko la watoto wa mitaani/watoto waishio kwenye mazingira magumu
- Mtoto anaweza kupoteza muelekeo kimasomo, hii ni sambamba na kushuka kwa taaluma yake au kuacha shule kabisa
- Mtoto anaweza kupatwa na msongo wa mawazo ulio juu ya uwezo wake, hivyo kupoteza furaha na kuwa mnyonge
Tukilitazama
jambo hili kwa upande wa pili; kuna wakati kutengana kwa wazazi kunaweza kuwa
na faida kwa pande zote (mzazi mmoja na watoto).
Kama
alivyoainisha mtaalamu wa masuala ya talaka, divorce Judith Wallerstein
kuwa ni jambo la busara kutengana kwa talaka endapo watoto watapata
mateso ya kihisia,kupigwa au kunyanyaswa kijinsia na mzazi mmoja, au mzazi
mmoja anapokuwa mlevi kupindukia na kusahau majukumu ya familia.
Jamii na wanandoa kwa ujumla
tujitaidi kudumisha mahusiano ili tuwalee watoto kwa pamoja hivyo kuepusha
ongezeko la watoto wasiokuwa na muelekeo, pia watoto wa mitaani.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Jumamosi, 22 Juni 2013
UBUNIFU: HUDUMA YA INTANETI BILA MALIPO NDANI YA “MATHREE” NCHINI KENYA…
Picha na http://www.bbc.co.uk/swahili: Daladala nchini Kenya, alimaharufu hujulikana kama "Mathree au Matatu" |
Kutokana na adha ya foleni jijini Nairobi nchini
Kenya, wafanyabiashara wa “Mathree” au “Matatu” wabuni njia mpya iliyo sanjari
na matumizi ya intaneti ili kuwapoza abiria na kuboreka.
Abiria akiwa ndani ya “Mathree” au “Matatu”
anaweza kusoma barua pepe pia kusoma habari kupitia mitandao mbalimbali.
Huduma hii imewavuta abiria wengi kukimbilia "Mathree" zenye "wiFi".
Sikiliza ushuhuda wa abiria kupitia:
Ijumaa, 21 Juni 2013
MTAZAMO: EPUKA KUWA NA MTAZAMO HASI…
Picha na hot100tips.com |
Mara
kwa mara watu wamekuwa na manung’uniko yaliyo sanjali na hali ngumu ya
maisha.Hii imewafanya wengi kukosa muelekeo na mwishowe kukata tamaa, hasa
waonapo wengine wakitesa na maisha.
Watu wamesongwa na kulaumu huku wakitumia
muda mwingi kusononeka bila kuchukua hatua ya kufikiri tofauti.Ijulikane kuwa
jinsi utumiavyo muda mrefu kusononeka na kunung’unika ndivyo unavyojiweka
kwenye nafasi kubwa ya kupoteza fursa nyeti za kukutoa kimaisha.
Yafuatayo ni baadhi tu ya madhara ya kuwa na mtazamo hasi
wa maisha;
- Utajiona huwezi kila kitu
- Utakuwa msindikizaji wa maamuzi ya watu, hutaamini maamuzi yako
- Utatofautiana na watu wenye mafanikio kifedha mfano; utachulia watu wote wenye fedha ni wezi ,mafisadi, na washirikina.
Mwandishi
maarufu, mfanyabiashara mkubwa nchini Marekani – Robert Kiyosaki
aliwahi
kusema;
“what you think it’s real, becomes
your reality” kwa lugha ya Kiswahili- “unachofikiri ni halisi kinakuwa uhalisia wako”akitoa mfano kuwa mtu akisema siwezi kuwa tajiri, mtazamo huu huwa halisi kwake
kwa sababu hatakuwa na juhudi zozote za kumpeleka hatua ya kuwa tajiri.
- Utapoteza fursa nyingi za kukutoa kimaisha
- Kukosa ujasiri na uthubutu wenye tija mfano mtu anaweza kusema “nikijaribu kufanya biashara hii nitapata hasara…anaweka uhakika wa kupata hasara kabla ya kuanza biashara yenyewe, hivyo kutothubutu.
Wakati mwingine nitajitahidi kukuletea mbinu
za kuwa na matazamo chanya. “JIFUNZE KUWA NA MTAZAMO CHANYA.” Ukitumia mbinu
hizo zitakubadilisha sana, hutakuwa kama ulivyokuwa.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Jumatano, 19 Juni 2013
ELIMU: MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO (TEHAMA) KUJIFUNZIA NI SULUHISHO LA ELIMU BORA TANZANIA…
Kufuatia mapinduzi
makubwa ya Sayansi na Teknolojia nchini na duniani kwa ujumla mambo mengi
yamerahisishwa sana.
Wakati huo huo, uzuri wa Teknolojia unaweza
kuleta hasara endapo hakutakuwa na uelewa sahihi wa matumizi.Mfano halisi ni
matumizi ya Intaneti kupitia simu za viganjani.Nilitegemea, hii ingekuwa ni
fursa kwetu watanzania kuwasaidia watoto wetu kujifunza kwa kupata maarifa
kupitia njia hiyo…kinyume chake wanajamii wanatumia intaneti “kuchat” na masuala yanayowahusu, pia kupitia
mitandao ya kijamii kwa mambo yasiyojenga.
Wakati huo huo wanasema walimu hawatoshi na
hawafundishi…je umewahi kuchukua jitihada kutafuta njia mbadala? au tunasubiri
majibu ya mwisho ya mtihani yatolewe ndiyo tushike vichwa na kutoa lawama kwa
Serikali na walimu wake?
Hapa inatakiwa ieleweke kuwa mafanikio ya
watoto wetu yanaanzia na sisi wazazi/walezi ikiwa sambamba na watoto wenyewe
kujitambua na kutii.
Naomba niwathibitishie kuwa kwa hatua
tuliyofikia kimawasiliano na teknolojia ya intaneti kupitia simu zetu, hakuna
kitu kisichokosekana mtandaoni kuhusiana na masomo ya watoto wetu. Kuna mwalimu
anaitwa Google, You tube…tuanze
kuwatumia.
Cha msingi ni kumnunulia mwanafunzi muongozo
wa kila somo”syllabus” na kusimamia kujifunza.Shule inakuwa ni sehemu ya kwenda
kuuliza maeneo asiyoelewa na kufanya mazoezi kujifua na kile alichojifunza.
Inafika hatua nashangaa sana kuona teknolojia
inabadilika kwa kasi na watu wanaipokea kwa kasi kinyume na matumizi hasa
kwenye nyanja hii nyeti ya kujielimisha.
Si kitu cha ajabu kumuona kijana/mwanafunzi
anatumia tabiti “tablet” kusikilizia
muziki, kuchati na marafiki na kutazama sinema…ukimuuliza maswali kuhusu
masomo ya shuleni anakujibu mwalimu hajafundisha bado.Hivi, tutamtegea mwalimu
kwa asilimia 100% hadi lini?
Hili linachangia
kwa asilimia nyingi idadi kubwa ya wanafunzi wa sekondari kufeli na wale
walio vyuo vikuu kukosa mbinu za utendaji katika soko la ajira. Bila shaka unauona
mwelekeo wa jahazi la elimu ya Tanzania…huna haja ya kuwa na Shahada ya
uzamili(Masters) au ile ya uzamivu(PhD) ili kujua hatima yake.
Nikiendelea sana, watu watasema nawapangia
matumizi ya simu na tabiti au komputa zao.Lakini uhalisia ndiyo huo.Tunatakiwa
kubadilika ili kulikomboa jahazi la elimu ya Tanzania.
Ukiwa ni mzazi/mlezi mwenye mapenzi mema na unataka
kumuandaa mwanao kusoma kuendana na teknolojia ya habari na
mawasialino, pia usiyetaka mizigo isiyo ya lazima hapo baadaye, chukua hatua sasa kumsaidia mwanao kielimu na kujitambua kabla maji hayajamwagika!
Unaweza kuwasiliana Jielimishe Kwanza! kwa ushauri zaidi.
Simu ya kiganjani: +255 754 572 143
Barua pepe:
jielimishekwanza@gmail.com
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Jumanne, 18 Juni 2013
UONGOZI BORA: HII NI SIRI KUBWA YA VIONGOZI WALIOFANIKIWA…
Raisi,(1994-1999), Mwanamapinduzi,Mpigania haki kuhusu ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini-Nelson Mandela. (Picha na www.newstimeafrica.com). Picha hii imewekwa kwa kuthamini mchango wake, ni mfano wa kiongozi bora wa kuigwa, pia kumtakia heri. |
Wataalam wa masuala ya uongozi wamekuwa
wakijiuliza swali lifuatalo mara nyingi; viongozi huzaliwa au hutengenezwa?
Ikimaanisha-ni mtu tu anajikuta kazaliwa ana uwezo wa kuongoza au anafundishwa
kuwa kiongozi?
Mtazamo wa wengi ni kuwa viongozi
wanazaliwa…ni kipaji tu cha mtu cha kuzaliwa nacho.Yaani, wakichukulia kuwa
tangu kipindi cha utoto utaiona tabia ya mtoto akiwaongoza wenzake katika
michezo ya kitoto.
Pia, kiasilia kunapokuwa na watu zaidi ya
wawili na wanahitaji kutoa maamuzi ya pamoja utaona kuwa mmoja hujiweka
kipaumbele katika kutoa maamuzi na anakubalika.
Mwandishi maarufu, Stephen R.Covey katika
kitabu chake cha “The 8th
Habit- From Effectiveness to Greatness” anapingana na mawazo ya wengi kwa
kuweka msimamo hasi…akimaanisha kuwa viongozi hawazaliwi wala hawatengenezwi ila
mazingira huwafundisha na kuwalea.
Akiunganisha na wazo la uwezo wa asili wa
mwanadamu…Stephen anasema; "kikawaida mwanadamu ana nguvu ya asili ya kufanya
chaguo."
Hivyo
basi, akasiliba kwa kusema "viongozi hujitengeneza
kwa kuchagua wenyewe", na endapo watafuata kanuni na kujiongezea nidhamu
dhabiti, uhuru wao wa kuchagua huongezeka.
Akithibitisha
ukweli wa wazo lake Stephen kwa kulinganisha na wazo la Dk.Noel Tichy ambaye
alisema;viongozi hawazaliwi ila hufundishwa…Stephen anaunganisha mawazo kwa
kusema; watu hutumia nguvu yao ya kuchagua kujifunza na kufuata mafunzo.
Tukifuatilia kwa makini orodha ya viongozi wenye mafanikio duniani ni kubwa.Nikisema nianze kumjadili mmoja hadi
mwingine itachukua muda mrefu sana bila ya kumaliza.Ila viongozi wote hawa
walikuwa na tabia/wana tabia za kipekee na zinazofanana ambazo ni;
1. Kuwa na maono”vision” ya mbali yenye tija na kuyafanyia utekelezaji, ambayo
wengine (wafuasi) hawayaoni. Mtaalamu wa masuala ya uongozi na mwandishi
aliyebobea nchini Marekani Warren Bennin alisema, “uongozi ni kubadilisha maono kuwa uhalisia”
2.
Hutenda kwa kufuata dhamiri “conscience”…hutenda kwa kufuata sauti
ya moyo ya ndani inayomfanya mtu kutofautisha jema na baya. Kama Stephen Covey
anavyosema; “Sauti hii ya ndani ni tulivu
na ya amani. Pia inahusisha kujitoa mzima mzima kwa jambo jema tarajiwa…Ni hii
dhamiri inayotafsiri maono kuwa huruma kwa wengine.”
3. Huwa
na shauku”passion” kubwa ya
kutenda.Hii hutoka moyoni. Nikimnukuu
mjasiriamali mwenye mafanikio na mwandishi wa vitabu Anthony Robbins anasema;
"There is no greatness without a
passion to be great, whether it's the aspiration of an athlete or an artist, a
scientist, a parent, or a businessperson." Akimaanisha kuwa hakuna ukuu au umaarufu unaokuja bila ya shauku ya
kuwa mkuu au maarufu, si ndoto ya kuwa mwanariadha au msanii, mwanasayansi,
mzazi au mfanyabiashara.Haya yote yanaanza na kuwa na shauku.
4.
Nidhamu”discipline”
kwao ni silaha.Kama alivyosema raisi wa
26 wa Taifa la Marekani Theodore
Roosevelt alisema; “kila kitu
kinawezekana kwa kuwa na nidhamu binafsi”
5. Ukifuatilia
mafundisho au hotuba zao, huongea na hisia za watu kwa kugusa mioyo. Hupangilia
maneno yao si kwa kujifurahisha wenyewe, bali kugusa hitaji la ndani la mioyo
ya wengine. Kwa mantiki hiyo, wafuasi hupenda kuwasikiliza na kutendea kazi
mawazo na mafundisho yao.
Bila shaka umepata kujua kuwa kila mtu anaweza kuwa
kiongozi.Pia ni suala la kuchagua kujifunza na kufuata kanuni za uongozi bora
na si bora kiongozi.
Jielimishe Kwanza!
Tutumie maoni yako
Barua
pepe:jielimishekwanza@gmail.com
Jumamosi, 15 Juni 2013
FAMILIA: SIKU YA BABA....
Picha na www.bagboys.net |
Ni siku kuu ya kutoa heshima kwa baba na kuheshimu umuhimu
wa baba katika jamii.Siku hii husheherekewa pande nyingi za dunia hasa katika siku Jumapili ya tatu ya mwezi Juni.Mwaka huu
imeangukia tarehe 16/06/2013.
Siku hii ilianzishwa nchini Marekani katika karne ya 20 ili
kuendana na Siku ya mama, pia kuonyesha na kukamilisha upendo kwa wazazi-baba
na mama.
Siku ya baba ilianzia
mjini Spokane,Washington katika eneo la YMCA mwaka 1910 na Sonora Smart Dodd,
aliyezaliwa Arkansas.
Ni vyema tukajumuika kuienzi siku hii muhimu ili kuthamini
uwepo na juhudi za baba kwenye familia na jamii kwa ujumla.
Soma zaidi: http://en.wikipedia.org/wiki/Father%27s_Day
Ijumaa, 14 Juni 2013
NUKUU MAARUFU: UNAWEZA KUJIONA WEWE UNA KIBURI NA KING'ANG'ANIZI KULIKO WENGINE...FUATILIA NUKUU MAARUFU ZA ROBERT MUGABE-RAISI WA ZIMBABWE! JILINGANISHE...
Raisi Robert Mugabe wa Zimbabwe.Picha na www.telegraph.co.uk |
UNAWEZA KUJIONA WEWE UNA KIBURI NA KING'ANG'ANIZI KULIKO WENGINE...FUATILIA NUKUU MAARUFU ZA ROBERT MUGABE-RAISI WA ZIMBABWE! JILINGANISHE...
PIA KWA TAARIFA ILIYOTOLEWA JANA-13 JUNI 2013, MUGABE AMETANGAZA RASMI KUGOMBEA URAISI KWA MARA NYINGINE-YAANI IWE MARA 33 MADARAKANI...
Zifuatazo ni nukuu maarufu za Raisi Robert Mugabe kama zilivyotolewa kwa lugha ya Kiingereza na www.brainyquote.com/quotes/authors/r/robert_mugabe.html#BdG8Mvci9r0QhfKu.99
Together, After, Vote
Our votes must go together with our guns. After all, any vote we shall have, shall have been the product of the gun. The gun which produces the vote should remain its security officer - its guarantor. The people's votes and the people's guns are always inseparable twins.
Robert Mugabe
Jesus, Once, Times
I have died many times. I have actually beaten Jesus Christ because he only died once.
Robert Mugabe
Mind, Europe, Banning
We don't mind having sanctions banning us from Europe. We are not Europeans.
Robert Mugabe
Africa, White, Indigenous
The white man is not indigenous to Africa. Africa is for Africans. Zimbabwe is for Zimbabweans.
Robert Mugabe
Keep, England, Zimbabwe
So, Blair keep your England, and let me keep my Zimbabwe.
Robert Mugabe
Fear, Heart, Enemy
Our party must continue to strike fear in the heart of the white man, our real enemy!
Robert Mugabe
Change, Themselves, Call
Countries such as the U.S. and Britain have taken it upon themselves to decide for us in the developing world, even to interfere in our domestic affairs and to bring about what they call regime change.
Robert Mugabe
Ask, Longer, Land
We are no longer going to ask for the land, but we are going to take it without negotiating.
Robert Mugabe
Equality, Happen, Country
The land is ours. It's not European and we have taken it, we have given it to the rightful people... Those of white extraction who happen to be in the country and are farming are welcome to do so, but they must do so on the basis of equality.
Robert Mugabe
Pride, Rather, Actually
We pride ourselves as being top, really, on the African ladder... We feel that we have actually been advancing rather than going backwards.
Robert Mugabe
Become, Lose, Choice
If the choice were made, one for us to lose our sovereignty and become a member of the Commonwealth or remain with our sovereignty and lose the membership of the Commonwealth, I would say let the Commonwealth go.
Robert Mugabe
Age, Human, Africa
We of Africa protest that, in this day and age, we should continue to be treated as lesser human beings than other races.
Robert Mugabe
May, Necessary, Methods
It may be necessary to use methods other than constitutional ones.
Robert Mugabe
Drink, Exercise, Eat
Don't drink at all, don't smoke, you must exercise and eat vegetables and fruit.
Robert Mugabe
Times, Started, Policy
In most recent times, as the West started being hostile to us, we deliberately declared a Look East policy.
Robert Mugabe
Country, Nation, Stay
Stay with us, please remain in this country and constitute a nation based on national unity.
Robert Mugabe
Food, Enough, Why
We are not hungry... Why foist this food upon us? We don't want to be choked. We have enough.
Robert Mugabe
History, Enough, Suffering
Was it not enough punishment and suffering in history that we were uprooted and made helpless slaves not only in new colonial outposts but also domestically.
Robert Mugabe
Oneself
There are things one must do for oneself.
Robert Mugabe
Making, Means, Ways
Some people are contriving ways and means of making us collapse.
Robert Mugabe
Done, Said, Step
We have said the first step was to designate the land, inform the owners. And the second would be to get the responses from the owners. And this will be openly done.
Robert Mugabe
Free, Vote, Anyone
People are free to campaign and they will be free to vote. There won't be any soldiers, you know, at the queues. Anyone who has the right to vote is free to go and cast his vote anywhere in his own area, in his own constituency.
Robert Mugabe
I wish to assure you that there can never be any return to the state of armed conflict which existed before our commitment to peace and the democratic process of election under the Lancaster House agreement.
Robert Mugabe
Read more at http://www.brainyquote.com/quotes/authors/r/robert_mugabe.html#BdG8Mvci9r0QhfKu.99
Imetolewa na,
Jielimishe Kwanza!
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)