ikiutazama mfumo wa elimu hasa kwa
nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara, umelenga sana katika ufaulu wa masomo ya kitaaluma ili mwanafunzi
aanze safari yake kujikomboa kimaisha bila kuangalia kipaji cha mwanafunzi
husika, ikimaanisha kuwa taaluma kwanza, kipaji baadaye.
Imezoeleka kuwa ili mtu afanikiwe
katika maisha yake ni lazima afaulu sana katika masomo yake awapo shuleni.Vipi
kuhusu kutambua na kukuza kipaji cha mtoto/mwanafunzi bila kuangalia masomo ya
kitaalamu? Ikiwa kuna ushahidi wa kutosha wa watu maarufu waliotumia vipaji vyao kujiajiri pia
kuajiri wengine, tunaweza kuliona hili kwa mtazamo mwingine chanya wa
mabadiliko katika elimu.
Ukiangalia nchi nyingi zilizoendelea
kiuchumi, hazijapuuza hata kidogo kipaji alichonacho
mtoto/mwanafunzi…wanaangalia kwanza akipendacho mtoto kulingana na kipaji
chake.Kuanzia hapo mtoto huanza kukuzwa kwa kujitambua na kunoa kipaji chake.
Masomo mengine ya utaalamu huchukuliwa
kama ziada.Mtazamo huu ni mzuri kwa sababu mtoto/mwanafunzi akishindwa
kufanikiwa katika masomo yake ya kawaida(masomo ya utaalamu), anajikita moja
kwa moja katika kuonyesha kipaji chake kilichonolewa.
Nikitoa mfano halisi nchini Tanzania,
wataalamu wa masula ya elimu wamekuwa na mtazamo kuwa ili mtoto afanikiwe
maishani ni lazima apate matokeo kuanzia daraja la I hadi la III.Kuna kundi la
wanafunzi wengine wa daraja IV na wale wa daraja 0…je vipi kuhusu hawa? Ni
kweli hawawezi kufanikiwa maishani? Vipi kama kutakuwa na utaratibu wa
kuchunguza na kutambua vipaji vyao ili vitumike kujiletea kipato?
Katika siku za hivi karibuni, nchini
Tanzania,Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ilitoa tamko la kubadili madaraja
na viwango vingine vya ufaulu.Lililokereketa umma wa wananchi na wataalamu
wengine wa masula ya elimu ni lile la kubadili jina tu la divisheni 0 kuwa
divisheni V.
Nikirejea mtazamo wa kisaikolojia,
mtoto/mwanafunzi akiambiwa kuwa wewe ni “sifuri” inamjenga kuwa katika dunia
hii yeye hawezi kufanya lolote akijilinganisha na wengine.
Mtazamo wa Jielimishe Kwanza! kuhusu
badiliko la divisheni sifuri kuwa divisheni V ni kwamba, badiliko la jina halitabadilisha alama la
kundi hilo bali ni kumpoza mwanafunzi kisaikolojia ili asijione kuwa hawezi
kabisa.Hivyo basi anaweza kufanya kitu kingine nje ya mfumo rasmi wa elimu
uliomtenga kitaaluma na si kipaji chake.
Imefika wakati muafaka wa kuhamasisha
wadau wote wa elimu kulitazama suala la kipaji cha mtoto/mwanafunzi kuwa
kipaumbele kabla ya masomo ya kitaaluma, pia ni vyema kumfundisha mtoto/mwanafunzi kwa kile alichonacho, anachokifahamu, anachoweza kufanya kwanza. Hii itamsaidia mtoto/mwanafunzi kuwa
na wigo mpana wa kufanya kile moyo wake unapenda kwa ufanisi mkubwa.
_______________________________
“Sometimes we fight who we are,
struggling against ourselves and our natures. But we must learn to accept who
we are and appreciate who we become. We must love ourselves for what and who we
are, and believe in our talents.” ― Harley King
________________________________________________________________________________
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!