inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumatatu, 30 Septemba 2013

MAZINGIRA: USIMAMIZI WA SHERIA ZA USAFI WA MAZINGIRA NA CHANGAMOTO ZAKE

-->
Kumekuwepo na jitihada kutoka Halmashauri mbali mbali jijini Dar es salaam katika suala zima la usimamiwaji wa sheria ndogo za usafi wa mazingira.

Jitihada hizo zote zimekuwa zikigonga mwamba kutokana na ushirikiano hafifu kutoka kwa wananchi. Hii inaonyesha kuwa uelewa wa wananchi ni mdogo kuhusu umuhimu wa sheria ndogo zinazowekwa kuhusu utunzaji wa mazingira.Pia usimamizi wa sheria hizo ni hafifu.

Tunathibitisha ukweli wa jambo hili kutokana na hali halisi ilivyo katika eneo lililopo pembezoni mwa barabara ya Ali Hassani Mwinyi jijini Dar es salaam kama lilivyotembelewa na Jielimishe Kwanza! kwa mara nyingine.

Picha kama ilivyotolewa kwenye taarifa ya awali: http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/09/mazingira-juhudi-na-changamoto-za.html

Itambulike kuwa eneo hili ni la mfano kwetu ili iwe changamoto kwa maeneo mengine nchini!
Imetolewa na 
Jielimishe Kwanza!

Jumatatu, 23 Septemba 2013

MALEZI NA FAMILIA: MWELEZE YAFUATAYO MTOTO WAKO KUHUSU SHULE…

Wazazi wengi wamekuwa wakipata wakati mgumu sana kuwaeleza watoto wao kuhusu shule na faida zake sanjari na mustakabali wa maisha ya watoto wao.
Picha na
changeyourfate.org 


Wazazi wengine wamefikia hatua ya kuwadanganya watoto wao kuwa “…mimi nilikuwa nashika nafasi ya kwanza darasani hadi namaliza shule…” hii haijalishi kwao kuwa wameenda shule au la! Kila mzazi anasema alikuwa anashika nafasi ya kwanza darasani…mh! Sijui nani alikuwa wa mwisho darasani? Naomba tusifikie hapo, kuna njia nyingine ya kuwaeleza watoto wetu kuhusu shule.
Picha na www.alltreatment.com


...Inafahamika fika kuwa wazazi wengi huitaji mabadiko au maboresho katika mfumo wa elimu, lakini hivyo hivyo wanaona umuhimu wa watoto wao kwenda shule...

Leo naomba uchukue hatua muhimu na rahisi kumueleza mtoto wako kuhusu shule kama ifuatavyo;
1.ELIMU NI HATUA ENDELEVU MAISHANI
Kwenda shule ni hatua mojawapo-lakini ni hatua ndogo sana.Ukiwa shule utajifunza mbinu mbali mbali…hii isikufanye ukaacha kujifunza masuala mengine uyapendayo.Ichukulie elimu kama chaguo la kuboresha kipaji chako(Tukiamini, pia ni uhalisia kuwa kila binadamu ana kipaji chake).

2.SHULE NI HATUA YA AWALI YA KUAJIRIWA.
Shule inakuandaa kujipatia kipato cha halali, lakini si lazima kukupatia mali.

3.TAMBUA KUWA SHULE NI SEHEMU YA KUFAULU NA KUFELI
Soma kwa bidii.Pata ujasiri wa kusonga mbele pale unapofaulu pia pata ujasiri wa kuinuka tena pale unapoanguka(Kufeli).

4.UKIANZA SHULE, JITOLEE KUMALIZA
Jifunze kupambana na changamoto mbali mbali bila ya kukata tamaa.Tambua kuwa shule ni sehemu ya changamoto.

5.SHULE NI SEHEMU MUHIMU YA KUPATA HABARI
Tambua kuwa walimu wako ni watafiti, tumia taarifa zao, uliza maswali…fanya majaribio ya mara kwa mara ukitumia taarifa hizo kulingana na kile unachokipenda.Fuatilia kwa kina taarifa hizo kuliko kutegemea kupata majibu sahihi wakati wote ili ufaulu mtihani.

6. NI VYEMA UKAONEKANA MJINGA KULIKO KUWA MJINGA
Kama huelewi jambo Fulani, ni vyema kuuliza ili kupata ufafanuzi.Mwalimu akihitaji mtu kujitolea, jitolee.Watu hujifunza zaidi kwa kushirikishwa kuliko kukaa kimya ili kuonekana mtulivu.Uwe tayari kufanya makosa-hii ni hatua ya awali ya kujifunza.Fanya makosa sana.Kuwa na heshima lakini mchangamfu!

7.CHUKULIA FAIDA YA KUWA MDOGO
Hatua ya utoto ina faida zake, muda wa kutosha hasa baada ya masomo.Tumia muda huo kudadisi masuala mbali mbali.

8.TAFUTA KUPATA MAJIBU SAHII…LAKINI USIISHIE HAPO!
Tafuta jibu analohitaji mwalimu, lakini hakikisha una majibu si chini ya mawili.Kuwa na uwezo wa kutafuta majibu zaidi kwa maswali na matatizo mbali mbali ni njia mojawapo ya kuwa na wigo mpana wa kutatua matatizo.Maisha bila machaguo ni rahisi sana kuwa taabu.

9.JIAMINI…
Kila mtu ana uwezo wa kuelewa na kupambanua.Alama zako darasani hazibashiri kile utakachoweza kufanya baada ya shule.Fuata ndoto yako haijalishi watu wanasema nini…

10.UPENDO WANGU KWAKO NI WA MILELE
Waambie watoto wako, haijalishi alama gani wanapata shuleni, wao ni wa muhimu kwako.Kumbuka kuwa shule ni kama mchezo wa kupata na kupoteza, lakini utawapenda milele.

Makala hii imeandaliwa na Jielimishe Kwanza! kwa kushirikiana na Kitabu kiitwacho “Be Rich and Happy” kilichoandikwa na Robert Kiyosaki- Sura ya 25, Ukurasa wa  259-261.


Jumamosi, 21 Septemba 2013

MATOKEO YA KINYANG'ANYILO CHA BLOG BORA 2013

Jielimishe Kwanza! inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wale wote waliopiga kura na wale wote ambao hawakupata nafasi ya kupiga kura.Hii ni heshima kubwa na ya thamani kubwa sana katika kuifanya "blog" yetu iboreshe huduma zaidi hasa kuhamasisha jamii kubadili mtazamo kuwa chanya ili kuona fursa.

The Best Inspiration Blog
1.Gospel Kitaa
http://gospelkitaa.blogspot.com/

2. Jielimishe Kwanza 
http://jielimishekwanza.blogspot.com/

3. Michuzi Blog
http://issamichuzi.blogspot.com/ 

SOMA ZAIDI HAPA: 
tanzanianblogawards.blogspot.com/2013/09/matokeo-ya-tanzanian-blog-awards-2013.html#more

MALEZI NA FAMILIA:NDOA KATIKA UMRI MDOGO...


-->
M
Picha na plancanada.ca
ara nyingi wasichana wenye umri mdogo wamekuwa wakiozeshwa kwa kushurutishwa na wazazi, pia ndugu wa karibu kama njia mojawapo ya kujiingizia kipato na mali.Huu umekuwa ni utaratibu uliozoeleka sana, na wengine kuchukulia kama sehemu ya utamaduni.







                                                                                                                                                        
Hali  hii isiyo ya kawaida inajitokeza sana katika nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara. Tabia hii mbaya isiyojali haki ya mtoto wa kike imesababishia wasichana wengi kukosa fursa za kuendelea kukua kifikra,pia kushindwa kuendelea na masomo.
Msichana asipopata mahitaji yote hayo muhimu itamfanya awe tegemezi katika maisha yake yote.Hivyo iwapo mtoto wa kike ataozwa katika umri mdogo kuna uewezekano mkubwa wa kutojua kusoma na kuandika au atakuwa amepata elimu ya kiwango cha chini, hali hiyo itamfanya awe mtu masikini na hataweza kujitetea katika maswala ya ngono na nyumbani ukizingatia kwamba mara yingi msichana anaozwa kwa mtu mwenye umri mkubwa mara mbili yake,  ambaye tayari amekuwa ni mzoefu.
Katika hali hii mtoto huyu wa kike anakuwa na uhusiano tegemezi,uhusiano ambao mara nyingi huwa ni uonevu hasa ukizingatia ukweli wa hali ya kiuchumi. Kwa ufupi matarajio juu ya mtoto wa kike yamedumaa na ndiyo maana watoto wa kike wanapata athari kubwa zaidi ukichulia  kuwa msichana huyu mdogo  anatakiwa atoke kutafuta,lakini pia aangalie familia na kumuhudumia mume, wakati mwingine kukosa haki ya kula matunda ya jasho lake kwa sababu ya ukatili wa mwanaume.
Binti ambaye ndiye mke, asiye na elimu ya uzazi anapata shida ya kutambua haki ya kumuwezesha yeye kupumzika baada ya kujifungua.Hili hupelekea kuwa na watoto wengi ambao ni vigumu
kuwahudumia, matokeo yake ni kuongezeka kwa watoto wa mitaani. Jamii inapaswa kutambua na kubadilika,kujua kuwa jinsia zote zina haki sawa,mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla wanapaswa kuheshimiwa na kupewa haki zao kama ilivyo kwa watoto wa kiume na wanaume.
Wasichana wadogo wanapaswa kulindwa na tatizo la ndoa za utotoni  pia kupewa fursa ya elimu.
Picha na plancanada.ca
Ndoa za umri mdogo siyo nzuri na hazitakiwi,madhara yake ni makubwa kuanzia kwenye familia na Taifa kwa ujumla.
Jielimishe Kwanza! Badilika!
Na Linda Kagemulo, 0654289805,
lindakagemulo@gmail.com
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!

MTAZAMO: SOMO KUPITIA MIMEA…TAFUTA FURSA UONEKANE!

-->

N
 apenda kushirikiana nawe msomaji wangu kuhusu uumbaji wa Mungu ukihusisha na maisha yetu ya kila siku. Aliumba viumbe hai na visivyo hai, pia alimweka mwanadamu kuwa mtawala wa hivyo vyote.

Kupitia utashi aliopewa mwanadamu, aliweza kubuni mbinu mbali za kuwatunza viumbe wengine…natumaini tunatimiza lengo la kuwatunza viumbe hao wengine wasio na utashi.Kama tumesahau basi tukumbuke kazi tuliyotumwa!

Tukirudi katika maisha ya kawaida tunayoishi, mwanadamu amekuwa akigundua vitu vingi ili kutatua changamoto zinazomzunguka.

Kama upo makini na mdadisi utagundua kuwa vitu vingi afanyavyo mwanadamu kwa ubunifu ni kama amedurufu kazi ya uumbaji wa Mungu.

Kuna mifano mingi ya kuangalia; chukulia muonekano wa umbo la chombo cha usafiri wa anga (ndege) kushabihiana na umbo la ndege arukaye, matoleo mengi ya magari yanayopagawisha watu na vyombo vingine vya usafiri hushabihiana sana na viumbe hai alivyoviweka Mungu.
Picha na www.hdwallpaperstop.com


Hapa naomba niseme kuwa hati miliki ya ubunifu wa mwanadamu anamiliki Mungu na si kama wengine wanavyojisifu na kutamba.

Leo naomba tujifunze kupitia mimea hasa kutafuta na kuziona fursa mbali mbali katika maisha.



Kisayansi, mimea hutegemea sana mwanga wa jua kujitengenezea chakula na kumea mwisho kufikia hatua ya kutunza viumbe hai wengine kama binadamu na wanyama.

Fuatilia kwa makini hatua ya awali ya kuanza kuchipua kwa mmea: mmea ulio katika mazingira mazuri ya kupata mwanga wa jua humea vizuri na kuzaa matunda.

Pia mimea iliyo katika mazingira magumu hujitengenezea mazingira kwa hali yeyote ile ili kuliona jua (FURSA). Mimea mingine hujitahidi kupanda juu ya mimea mingine ili kuliona jua (FURSA). Je, mimea ina akili sana kushinda sisi? La hasha!

Mimea iliyo songwasongwa na magugu na kushindwa kujinasua kupata mwanga wa  jua (FURSA) hudumaa na mwisho kufa.

Je, mimea ina akili sana kushinda sisi? La hasha!

Tuhangaikie suala zima la kuziona fursa kwa hali yeyote ile ili tusife kifikra na kiiuchumi kwa kujifunza kupitia mimea.

Imetolewa na

Jielimishe Kwanza!

Jumatano, 18 Septemba 2013

NGUVU YA VIJANA KULETA MABADILIKO...



N
imeona tushirikiane kwa pamoja kuitazama nguvu ya vijana hasa waliopata fursa ya elimu kujitoa kusaidia jamii katika eneo la watoto yatima hasa waishio katika mazingira magumu.

Kuna kipindi nilishangazwa kuona wahitimu kutoka nchi zilizoendelea kuchangisha kiwango cha chini cha shilingi 1000/= eneo la Mlimani City jijini Dar es salaam kwa lengo la kusaidia watoto yatima.
Nilijiuliza, hili ndilo lengo la kuja nchini? au kuna agenda nyingine ya siri? Nilichukulia kama changamoto kwa upande mwingine…endapo nguvu ya vijana na wanajamii kwa ujumla ikitambua umuhimu wa kuchangia kwa ajili ya vituo vya watoto yatima, tunaweza kupunguza tatizo bila kutegemea misaada kutoka nchi za nje.
Jielimishe Kwanza! iliiona nguvu ya vijana wahitimu wa vyuo vikuu kutoka Kikundi cha Lugalo Graduates' Network(LG-Network 2001) ikionekana kwa mchango wao wa dhati kwa watoto yatima.

Ijumaa, 13 Septemba 2013

MJASIRIAMALI: WANAOKUPINGA, KUKUDHARAU,KUKUWEKEA VIKWAZO NA KUKUKEJELI WANAKUJENGA BILA WEWE NA WAO KUJIJUA…

-->
Najua jinsi inavyouma au kukatisha tamaa unapokuwa na wazo lako la biashara unaloliamini sana kukutoa kimaisha. Imezoeleka sana kwa watu kupenda kuwashirikisha ndugu, marafiki au jamaa wa karibu malengo yao ya biashara.Yafuatayo ni baadhi ya majibu wanayopata wajasiriamali wachanga mara tu baada ya kueleza nia zao za kuanzisha biashara;

·      Mh! Yalimshinda…………utaweza wewe?

·      Hivi nani kakwambia biashara hiyo inalipa kwa sasa!

·      Huogopi kupata hasara? Wengi sana wameporomoka na hiyo biashara!

·      Hiyo biashara inahitaji mtaji mkubwa sana, hakika hutaimudu!

·      Utapata wapi mtaji?

·      Hebu acha kupoteza muda wako…

Bila shaka maswali haya yanakatisha tamaa na kukupa hasira.Naomba nikufumbue macho ndugu msomaji…hasira hiyo ndiyo inayokufanya uboreshe sehemu zote zenye mapungufu katika wazo lako la biashara.

Hivyo, hupaswi kugombana wala kurumbana na kundi hilo linalokupa changamoto.Suala la msingi ni kutulia, kushusha pumzi, hasira zetu na kuwasikiliza kwa makini na kuwa wajanja kung’amua sehemu zenye mapungufu na kuboresha.

Faida nyingine ya kundi hilo linalotoa changamoto ni kukupa msukumo wa kusonga mbele na kukupa hasira ya kumiliki vitu binafsi.
Jaribu kufanya utafiti mwenyewe utakubaliana nami na hata kuamua kunipigia simu +255 754 572 143.
Ukiona watu wanakupongeza na kukubali kila unachowaambia…kuna walakini!

“I like oppositions and criticism ,they make me behave better with perfection-Henry Kazula.
USIOGOPE VIKWAZO, KUPINGWA...CHUKULIA HALI HIYO KAMA SEHEMU YA KUJIJENGA ZAIDI, UKIBORESHA UTENDAJI WAKO!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!


Jumatano, 11 Septemba 2013

MAZINGIRA: JUHUDI NA CHANGAMOTO ZA USIMAMIZI WA SHERIA NDOGO ZA UTUNZAJI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA…


Katika pita pita za kuchunguza usimamizi wa sheria ndogo za kulinda na kutunza mazingira zinazowekwa na Halmashauri mbali mbali kwa ushirikiano wa wananchi nchini Tanzania, Jielimishe Kwanza! ilifanikiwa kujionea hali isiyo ya kawaida pembezoni mwa bara bara ya Ali Hassani Mwinyi jijini Dar es salaam. 

Pichani ni bango linalojieleza vizuri kabisa…ikiwa ni amri kutoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kudhibiti utupaji ovyo taka katika eneo husika.
Kuna maswali ya msingi ya kujiuliza…je, matangazo/vibao vya kutoa onyo vinaendana na utekelezaji? Je, kuna ufuatiliaji/usimamiaji wa sheria  mara tu baada ya kuweka vibao/matangazo ya onyo?Au ni wakati gani sheria hizo ndogo huwa na meno?...usiku au mchana?...wakati wa ugeni mkubwa au la? Hapo unaweza kulinganisha matokeo ya ukiukwaji au utekelezwaji wa sheria hizo ndogo.

Ifahamike kuwa, kama hakuna ufuatiliaji/utekelezaji wa onyo zinazotolewa, hali huwa mbaya zaidi ya mwanzo…mwanadamu akipewa onyo halafu asione utendaji/madhara ya kukiuka  onyo, hupuuzia onyo hilo na kuchukulia hali kimazoea.

Ushauri wetu namba 1, tunashauri...mabango/vibao vya onyo vieleze aina ya adhabu atakayopata mtupaji taka katika eneo husika…Hasa adhabu ya fedha taslimu.Pia ni vyema kutumia ufuatiliaji shirikishi/jamii kwa kutoa motisha ya nusu ya fedha taslimu itolewayo kama adhabu kwa watoa taarifa ya uchafuzi wowote wa mazingira.Hii inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa mtoa taarifa na Halmashauri husika kwa ujumla wakati huo huo jiji liking'ara.
 
 Ushauri wetu namba 2, tunashauri kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya kutupa taka na kuwe na ufuatiliaji wa mara kwa mara kuhakikisha taka hazirundikani kwa muda mrefu.Kwa kutumia mapato ya ushauri namba 1...yanaweza kuboresha huduma ya ushauri namba 2.
 
 
Soma mfano wa kuigwa wa mbinu za kuhifadhi mazingira kupitia mji wa Moshi uliofanikiwa katika kusimamia sheria ndogo ya uhifadhi wa mazingira http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/08/mazingira-hii-ndiyo-siri-ya-usafi-wa.html
 
 
Jamii kwa ujumla inapaswa kujua uhalifu na uchafuzi wa mazingira wa aina yoyote ile una athari kubwa kwa kila mwanadamu...tushirikiane kwa pamoja kuipendezesha dunia hii inayotutunza.

 
Imetolewa na,
Jielimishe Kwanza!
Kwa kuthamini umuhimu wa mazingira safi kwa afya bora!
 


Jumanne, 10 Septemba 2013

MTAZAMO: HIVI NDIVYO TUNAVYOWEZA KUONDOKANA NA UTUMWA WA KIFIKRA UNAOPELEKEA UMASIKINI…

-->
Nikianza kwa kumnukuu mwanamuziki maarufu wa "Reggae" dunia-Hayati Nesta Robert Marley almaarufu “Bob Marley” aliwahi kusema katika sehemu ya wimbo wa “Redemption Song” kuwa “Emancipate yourselves from mental slavery; None but ourselves can free our mind.” Akiweka msisitizo huo kuwa hakuna mtu mwingine anayeweza kutukomboa/kukukomboa kifikra isipokuwa sisi wenyewe…au wewe mwenyewe. ANGALIA VIDEO NA MASHAIRI YA WIMBO HUO KUPITIA
Kama utatafakari kwa kina utagundua kuwa walio juu kimaendeleo na wenye upeo wa kupambanua mambo hupenda kuwakandamiza walio chini hasa wazubavu na hata kudiriki kupita juu ya vichwa vyao.
Hata siku moja hawawapi nafasi walio chini kuchomoza kimaisha, hasa kwa kuwapa msaada ili waweze kufikiri vizuri na kutenda sawia na wenyewe wanavyotenda.
Hali hii hupelekea kuongezeka kwa wimbi kubwa la wasio nacho na kuimarika kwa kundi la walionacho. Sina hakika kama lengo la Mungu kumuumba mwanadamu ni kuwa masikini…la hasha! Nini husababisha haya yote?
Wabudha wana msemo wao maarufu sana ulio na uhalisia kuwa “What we think, we become.” Wakimaanisha-kwa tafsiri isiyo rasmi kuwa, tunanyoonekana na jinsi tulivyo kimaisha ni kutokana na mawazo yetu.Mfano, tukiendelea kunung'unika sana kuwa nchi hii ni masikini sana na hali kuna rasilimali nyingi hadi wengine wanakuja kugombania…ndivyo ilivyo na itakavyokuwa!
Kiujasiri kabisa, ndugu msomaji, nikutie moyo kuwa tukibadili mtazamo wetu wa kufikiri na kuepukana na utegemezi wa kufikiri tutaondoka hapo tulipo…hivyo kuacha kuimba wimbo huu wa “Nchi yetu ni masikini sana” ambao walio nacho wanaupenda sana kuuimba na kuucheza wakati huo huo wengine-wasio nacho kusikia kelele ndani ya masikio yao na kusononeka mioyo yao.
Tunatakiwa kuamini, kufikiri tofauti na kuangalia tulicho nacho kwanza-mfano kipaji au uwezo wa asili tuliopewa na Mungu kuwa kianzio cha mtaji wetu sambamba na kulinganisha na rasilimali tulizo nazo kusonga mbele.Kuna uthibitisho kutoka kwa wengine walioiona siri hii ya kutumia kile walicho nacho kwanza. Jielimishe Kwanza! Jitambue! Fuatilia! Simamia kwa kutenda!
Tusipende kuwa bendera fuata upepo na kutumika na hao wanaotukandamiza…hata siku moja hawawezi kutukomboa kifikra.
Huu ni mtazamo wa Jielimsihe Kwanza! Tunakutakia kila la heri katika kubadili mtazamo kuwa chanya!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumatatu, 9 Septemba 2013

Tanzanian Blog Awards: Mwisho wa Kupiga Kura ni 9/15/2013

Tanzanian Blog Awards: Mwisho wa Kupiga Kura ni 9/15/2013

HATUA YA MWISHO YA KUPIGA KURA. MWISHO NI TAREHE 15/9/2013.

http://tanzanianblogawards.blogspot.com/


TUNATHAMINI SANA MCHANGO WAKO WA KUIPENDEKEZA BLOG YAKO UIPENDAYO www.jielimishekwanza.blogspot.com NA KUIFANIKISHA KUINGIA KATIKA ORODHA YA BLOG ZINAZOWANIA TUZO BORA KWA MWAKA 2013.

TUNAKUOMBA TENA UICHAGUE BLOG YAKO www.jielimishekwanza.blogspot.com KUWA BLOG BORA KWA MWAKA 2013 KATIKA VIPENGELE TEULE KWA KUFUATA LINK ZIFUATAZO KUPIGA YAKO:-

TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO, NAJUA UNAPIGA KURA KWA MANUFAA YA WATANZANIA WOTE NA KUIENZI LUGHA ADHIMU YA KISWAHILI.

TUNAAHIDI KUKULETEA MAMBO MAZURI ZAIDI YA HAPA KADRI SIKU ZINAVYOENDELEA.
KARIBU...TUJIELIMISHE PAMOJA!

Imetolewa na
Mkurugenzi mtendaji,
Jielimishe Kwanza!

Alhamisi, 5 Septemba 2013

MTAZAMO: TUNZA RASILIMALI MUDA KWA MANUFAA!

-->
Picha na www.empowernetwork.com
Kumekuwa na mazoea kwa jamii za watu wengi hasa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kuchukulia suala la kutunza rasimali muda kama mzaha au kitu fulani cha kuchezea na kupuuzia. Hili ni tatizo, lazima tukubaliane kutokukubalina! ili kubadili mtazamo uliopo.
Nilipoanza kujifunza jinsi ya kutunza muda kupitia watu wanaotunza muda na kujisomea vitabu mbali mbali niligundua siri kubwa katika utunzaji rasilimali muda.Kwa sasa naweza kufanya mambo mengi katika ratiba niliyojiwekea.Nimetenga muda maalum pia kukuandikia ndugu msomaji ili nawe upate kupona na ugonjwa huu ambao unaonekana ni wa kawaida ilihali unateketeza uchumi wa mtu mmoja na taifa kwa ujumla.

Ifahamike kuwa muda ni rasimali kama rasimali nyingine mfano madini…endapo utatumika vibaya ni dhahili kabisa tutarudi kwenye ule usemi usemao “majuto ni mjukuu.”

Nikichukulia mfano jijini Dar es salaam nchini Tanzania, utakutana na watu wenye visingizio kadha wa kadha kuhusiana na utunzaji wa muda…wengi wamekuwa wakichelewa kuripoti kazini na kusababisha huduma nyingi kutotolewa kwa wakati, kubwa likiwa foleni barabarani.

Unaweza kuweka ahadi na mtu akiwa yeye ndiye alipendekeza muda na siku wa kukutana, chakushangaza anakuwa wa kwanza kuchelewa kufika eneo la ahadi na kuanza kutoa visingizio.

Pia kuna makundi ya watu wengine wajulikanao kama wapoteza muda…wanajisifu kabisa kwa kusema; ah! tupo hapa tu tunapoteza poteza muda.” Wengine wanatumia muda vibaya kwa kupiga soga na kusengenya wengine.

Tunaweza kuhama hapo kwa  kufuata na kufanya mambo 10 yafuatayo:

1. JIWEKEE MPANGO WA SIKU WENYE MANUFAA UNAOWEZA KUUTEKELEZA KWA WAKATI HUSIKA


2.  TAMBUA KUWA RATIBA YA KESHO HAIPANGWI KESHO ASUBUHI…INAPANGWA KABLA YA KULALA

3.  TUMIA SIMU YAKO KUKUKUMBUSHA MAJUKUMU YA SIKU NA MUDA HUSIKA

4.  UNAPOWEKA AHADI NA MTU HAKIKISHA UMETATHIMINI MUDA UTAKAOTUMIKA UKIWA NJIANI…UTAEPUKA KUSINGIZIA FOLENI

5.   JIJENGEE HALI YA UAMINIFU KATIKA KUTIMIZA AHADI KWA WAKATI

6.    JIJENGEE TABIA KUSOMA VITABU VYENYE MANUFAA ILI KUEPUKANA NA KUPIGA SOGA

7.    THAMINI MUDA WA WENGINE…TAMBUA KUWA WANA MAJUKUMU

8. TAMBUA KUWA UNAPOHARIBU RATIBA YA MTU MMOJA UMESABABISHA WATU WENGINE WENGI KUHARIBU RATIBA ZAO

9.     KUWA MTU WA MFANO KUJALI MUDA MARA KWA MARA, WENGINE WATAKUIGA

10. USIAMINI SANA KUHUSU DHARULA…EPUKA KUHAIRISHA HAIRISHA MAMBO YALIYOPANGWA

Nakutakia mafanikio mema katika kuwa mtu wa kutunza rasilimali muda kwa manufaa yako na wengine.

Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!