inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Jumatatu, 28 Oktoba 2013

KAZI NA AJIRA: HIVI NI VIASHIRIA VYA UTUMWA WA KISASA (MODERN-DAY SLAVERY)


H
 uu ni muendelezo wa makala ya Jumatatu 21 Octoba 2013 
http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/10/ajira-na-kazi-jiepushe-zuia-utumwa-wa.html ikiwa na lengo mahsusi la kuainisha viashiria vya utumwa wa kisasa katika maeneo mbali mbali ya kazi. Mwisho wa yote ni wewe utakayejiweka katika kundi husika na kuangalia jinsi ya kuendana na mazingira halisi ya kazi uliyonayo.

Austin Choi-Fitzpatrick (2008)[1] alianisha viashiria vya utumwa wa kisasa. Alisema, mfanyakazi aweza kuwa mtumishi wa ndani, mfanyakazi wa mgahawa, mkulima,muuza duka, mfanyakazi kiwandani, au mwanamke/mwanaume anayeuza mwili wake. Katika makundi yote ya wafanyakazi, mfanyakazi aweza kuwa mtumwa endapo;
  •      Anatumikishwa na kushikiliwa kinyume na matakwa yake
  •      Hawezi/ hayupo huru kubadilisha mwajiri
  •      Hawezi kudhibiti mshahara wake 
  •      Ni vigumu kuondoka katika eneo lake la kazi kwa sababu ya kufuatiliwa
  •      Ni vigumu kujielezea au kujiweka wazi mbele ya watu kuhusu kazi yake
  •      Anatishwa pale anapotaka kuacha kufanya kazi
  •      Amedanganywa kuhusu malipo/ mshahara wake
  •      Nyaraka zake muhimu kuhusu kazi au hati ya kusafiria imeshikiliwa ili aendelee kuwepo kazini
Yawezekana umekuwa ukifanya au kufanyiwa moja ya viashiria tajwa bila kujua.Hivyo basi, lengo la makala hii kupitia Jielimishe Kwanza! ni kukuhamasisha kujitambua na kuchukua hatua ya kubadili mtazamo ili kuboresha kipato chako na kuongeza ufanisi katika maeneo ya kazi.

Soma na hii kujua zaidi kuhusu viashiria vya utumwa wa kisasa http://www.antislavery.org/english/slavery_today/what_is_modern_slavery.aspx


Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!

Jumapili, 27 Oktoba 2013

ELIMU: MTAZAMO WA KISAIKOLOJIA KUHUSU ADHABU YA VIBOKO MASHULENI



Tunapolitazama suala zima la adhabu mashuleni nchini Tanzania na nchi nyingine duniani ni kizungumkuti.Kuna mgawanyiko wa kimtazamo na pia kiitikadi katika makundi mawili; kuna wale wanaosema ni vyema na wajibu wanafunzi wakapata adhabu pale wanapokiuka sheria za shule na wale wanapinga vikali kuwepo kwa adhabu ya aina yeyote ile kwa mwanafunzi(wakisisitiza kutoa maelekezo sahihi kwa mwanafunzi).



Picha na voices.yahoo.com
Kuna adhabu mbalimbali zilizozoeleka kwa miaka mingi iliyopita hadi leo.Kila aliyepitia shule kwa ngazi ya awali hadi sekondari anajua mojawapo ya adhabu hizo; kubwa kuliko zote, na iliyozoeleka, pia inayosemekana ni rahisi kuitumia kurekebisha tabia mbaya ni ile ya viboko…najua kila mtu atakuwa anakumbuka siku alipowahi kuchapwa viboko na mwalimu wake.Bila shaka hakikuwa kipindi kizuri kwako.



Nchini Tanzania, adhabu ya viboko inaendelea kwa kusimamiwa na sheria ya adhabu ya  Kitaifa ya mwaka 1979 kama ilivyotolewa katika kipengele cha 60 cha Sheria ya Kitaifa ya Elimu ya mwaka 1978.



Mwaka 2000, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliweka mkazo kwa kutoa tamko la kisheria kupunguza idadi ya viboko kwa wanafunzi kutoka 6 hadi 4 na ilisisitiza kuwa ni Wakuu wa shule pekee wanaotakiwa kutoa adhabu hiyo.Pia ilitoa tamko la kutoa adhabu kali kwa walimu watakao kiuka sheria hiyo.[1]



Kwa upande mwingine, sheria ya kuwalinda watoto ya mwaka 2009 inaeleza kuwa wazazi wana wajibu wa kuwalinda watoto wao dhidi ya uonevu wa aina yeyote ile(kipengele cha 9), ikijumuisha kupigwa kunakopelekea maumivu kwa mtoto (kipengele cha 3).[2]



Kisaikolojia, adhabu ya viboko kwa mwanafunzi inapingwa vikali kutokana na athari za moja kwa moja kwa mwanafunzi kama;
  • Zinatengeneza mahusiano mabaya ya kibinadamu
  • Huchochea hofu na hali ya kutotaka kutenda kwa mwanafunzi husika 
  • Huchochea hali ya kujitengenezea mbinu za kujikinga na adhabu
  • Madhala ya viboko ni ya muda…maumivu ya viboko hudumu muda mfupi
  • Hazichochei tabia njema bali zinaficha uovu na utukutu.Kawaida mwanafunzi au mtoto    anayechapwa sana viboko, huwa na tabia mbaya.

  • Huangalia zaidi makosa/tabia mbaya kuliko tabia njema
  • Adhabu hii haidhibiti chanzo cha kutokea tabia mbaya ya mwanafunzi.


Tuungane pamoja kipindi kingine katika ukurasa huu wa Elimu ili kujifunza mbinu mbadala wa viboko kwa kutumia saikolojia bila kuleta maumivu au madhara kwa mwanafunzi wakati huo huo ikiboresha tabia njema na ufaulu wake.



Imetayarishwa na kutolewa na

Jielimishe Kwanza!

Jumatatu, 21 Oktoba 2013

AJIRA NA KAZI: JIEPUSHE! ZUIA! UTUMWA WA KISASA…

Kabla ya kukoma kwa biashara ya utumwa mnamo karne ya 18, binadamu alikuwa akiuzwa kutoka nchi moja hadi nyingine(mfano Afrika kwenda Ulaya na Uarabuni) kwa lengo la kuwatumikia wengine kwa ujira mdogo sana au bila ujira kabisa.
Mara tu baada ya kukoma kwa biashara hiyo ya watumwa, wafanyabiashara na watu wa kada nyingine za ajira walikaa chini na kutafakari…mwisho wakaweka kitu kinachoitwa ujira/mshahara kulingana na utendaji au ubora auletao mwajiriwa katika eneo la kazi.Hapa kukatokea ngazi/madaraja mbali mbali ya mishahara!  

Nikimnukuu Jim Rohn aliyekuwa mwandishi maarufu na msemaji wa hadhara nchini Marekani- anasema; “People get paid by bringing value to the market place”.(Watu hulipwa kutokana na ubora wanaouweka katika soko)-Alizungumzia soko kama watu au eneo la kazi kwa kuwatumikia watu.

Kama ulikuwa hujui hilo, funguka macho ndugu msomaji.Hiyo ndiyo hali halisi.Hivyo basi ukiona unalipwa kidogo ujue una mchango mdogo sana kwenye soko.Hili limepelekea watu wengi sasa kuishi katika utumwa ulioboreshwa/Utumwa wa kisasa au kwa lugha ya Kiingereza “Modern-day Slavery”.
Picha na www.cvent.com
______________________________________________________________________________________________________________

Utumwa huu wa kisasa unahusisha; usafirishwaji wa binadamu ndani au nje ya nchi (aina hii ni kama inaturudisha tulikotoka-Kihistoria),watumishi wa ndani, kuzidiwa na madeni,kulazimishwa kuomba omba, kushurutishwa kimapenzi, kulazimishwa kuolewa katika umri mdogo, kunyanyaswa kijinsia na manyanyaso katika sehemu za kazi(kufanyishwa kazi ngumu kwa ujira mdogo au bila ujira kabisa).
______________________________________________________________________________________________________________

Nimeamua kukujuza hili kwa kulinganisha na taarifa ya gazeti la “The Citizen” –Jumamosi, 19 Octoba 2013 la nchini Tanzania kuripoti kuwa zaidi ya watu 300,000 nchini Tanzania ni watumwa katika mfumo huo wa utumwa wa kisasa!Tanzania ikiwa inaongoza kuwa na idadi kubwa ya watu walio katika utumwa wa kisasa katika nchi za Afrika Mashariki.

Kulingana na takwimu za mwaka 2013 za “Global Slavery Index” zinaeleza kuwa kati ya watu 310,000 hadi 350,000 wanaishi kama watumwa.Namba kubwa ya watu ikiwa mjini.Tanzania ikiwa ya 29 katika nchi 162 zilizofanyiwa utafiti huo duniani. Gazeti la “The Citizen” limeripoti.  Soma hii                                                        


Utumwa huu wa kisasa una viashiria vingi ambavyo nitavieleza siku nyingine.Pia tutafahamishana mbinu za kuepukana na utumwa huu wa kisasa hasa katika maeneo ya rasmi ya kazi.

Hivyo endelea kuifuatilia blog yako Jielimishe Kwanza! Ujielimishe! zaidi kwa Kuhamasika! Pia Kuhamasisha! wengine kubadili mtazamo ili kuepuka manung’uniko na kuwa na mtazamo chanya.
Soma na hii kujua zaidi kuhusu utumwa wa kisasa http://www.antislavery.org/english/slavery_today/what_is_modern_slavery.aspx

Imetayarishwa na kutolewa na,

Jielimishe Kwanza!








Ijumaa, 18 Oktoba 2013

TEKNOLOJIA: “Mozilla Firefox Aurora” KWA LUGHA YA KISWAHILI



Picha na descargar.info
Hivi ndivyo unavyoweza kutumia  “browser“ mpya ya “Mozilla Firefox  Aurora” kwa Kiswahili na Lugha nyingine unayotumia.



2.Nenda eneo la kutafuta, chagua lugha unayotumia, mfano: Kiswahili/ Swahili.

3.Shusha "Mozilla Firefox aurora" kulingana na uhitaji wa “computer" yako.
 
4.Fanya “Installation” ya kifurushi kipya cha “Firefox Aurora”kwenye computer yako.

5.Tambua kuwa huwezi kutumia “Mozilla Firefox” na “Mozilla firefox  Aurora” kwa wakati mmoja. Unapaswa kuifunga mojawapo unapotaka kutumia nyingine.

4. Furahia matumizi ya “Mozilla firefox  Aurora” kwa Lugha uipendayo.

UKIPATA TATIZO, TUWASILIANE .
Imetolewa na,
KWA KUTHAMINI, NA KUENZI LUGHA YA KISWAHILI.

Jumanne, 15 Oktoba 2013

MTAZAMO: SIMU YAKO NI IPI KATI YA HIZI?


W
 abunifu wa simu za mkononi wamekuwa wajanja sana kwa kucheza na fikra na mtazamo wa watumiaji. Ukiangalia kwa makini lengo la simu hizo linabaki pale pale-KUWASILIANA! haijalishi ni simu ya aina gani-iwe ya gharama kubwa au ndogo.


Katika kipindi kifupi wabunifu hao wamefanikiwa kuteka fikra za watumiaji wengi duniani kwa kuongezea vikolombwezo mbali mbali vya matumizi kama vile “Internet”, mfumo wa kutumia ujumbe wa moja kwa moja kama Whatsup! Na mengineyo yanayowapendezesha watumiaji kama kioo cha kugusa (kubonyeza ni shida!) na muonekano mzima wa simu.
Maboresho hayo ya simu kulingana na mitindo ya yote niliyotaja hujumuisha ongezeko la gharama -( mfano kuna simu inayofikia hadi Shilingi milioni mbili za Kitanzania).
Kulingana na mvuto wa simu hizo, makundi yote ya watu kiuchumi yamekuwa yakivutika kwa kasi kununua simu hizo za gharama kubwa.Yaani kwa lugha nyingine watu wameamua kufanya uwekezaji katika simu zao za mkononi.Bila kujua, watu wamesahau lile lengo la msingi la simu za mkononi la KUWASILIANA!
Ni kawaida kabisa kumuona mtumiaji wa simu, akimiliki simu zaidi ya moja zenye gharama kubwa…wakati huo huo maisha yake yakiwa duni.
Taarifa za hivi karibuni kutoka nchini Denmark na nchi nyingine za Ulaya zimethibitisha kuwa watu wamekumbwa na msongo wa mawazo kutokana na simu zao za mkononi “smartphone” (hasa kutumia muda mrefu kuperuzi kupitia mitandao ya kijamii -facebook, twitter n.k) pia kutokana na wimbi kubwa la mabadiliko ya teknolojia sanjali na simu za mkononi “smartphone” wakati huo huo wakitakiwa kufanya kazi na kuwasiliana na watu wanaowapigia simu. Kwa sasa baadhi ya watumiaji wengine wa simu hizo wameanza kurudia tena kutumia simu zenye matumizi rahisi.
Pia soma hii http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/jamii-na-mawasiliano.html uone simu za mkononi zilipotufikisha.
Ushauri wa bure: 
Ni vyema kuchukua hatua ya kujiuliza maswali haya ya msingi kabla ya kuwa na wazo la kununua simu mpya; 
  • Nanunua simu hii ili na mimi nionekane ninazo ilihali sina pesa?
  •  Nawekeza kiasi gani cha pesa kwenye simu yangu? Je, simu hii itakuwa inarudisha faida au itakuwa rasilimali isiyozalisha na yenye kutoa pesa mfukoni mwangu mara kwa mara?
  •  Simu ninayonunua itanisaidia kwenye masuala ya kazi na biashara kwa kuongeza ufanisi na kipato?
Huu ndiyo uhalisia, ni mtazamo tu! Tuangalie sana, tunapaswa kuwekeza kwenye mipango endelevu ya maendeleo na si kwenye mitindo ya simu inayoingia kila kukicha. Lakini siyo mbaya kama unawekeza kwenye simu yako bila kusahau maendeleo endelevu ya kijamii. 

Soma hii http://www.medscape.com/viewarticle/804666 pia kujua zaidi kuhusu matumizi ya "Smartphone".
Imetolewa na 


Alhamisi, 10 Oktoba 2013

VIJANA: KUJITOLEA - NJIA KUELEKEA KUPATA AJIRA NA UZOEFU WA KAZI


D
 hana ya KUJITOLEA inaonekana ni mpya sana kwa nchi mbali mbali za Kiafrika.Nikichulia mfano nchini Tanzania, vijana wengi wenye sifa za kupata ajira wanakaa nyumbani kusubiri wajibiwe maombi waliyotuma katika taasisi mbali mbali zinazotegemewa sana kwa kutoa ajira. Wakati huo huo wanasahau kuwa ujuzi wao unaendelea kupungua siku hadi siku. Pia kuna vijana wengine wasio na elimu ya kazi ila wana vipaji wapo vijiweni wakiendelea kufifisha vipaji vyao.

Jielimishe Kwanza! imefuatilia kwa kina dhana ya nzima ya KUJITOLEA na kuona kuwa kuna faida nyingi zinazoweza kupatikana kwa kijana kuchukua hatua ya uthubutu kuanza KUJITOLEA.Faida hizo ni; 

  1.      Kupata uzoefu wa kazi unayofanya…hivyo kigezo cha uzoefu kazini haikitakuwa kikwazo cha wewe kupata kazi
  2.       Utajifunza mbinu mpya za kazi
  3.       Kujiongezea wigo wa kufahamiana na watu katika kazi unayofanya
  4.      Ni njia mojawapo kukuunganisha na kazi nyingine
  5.      Utaifurahia kazi unayofanya kwa sababu unaipenda
  6.       Unajiongezea hali ya kuaminika kupata kazi

http://lindsayolson.com/5-reasons-you-should-volunteer-to-find-a-job/
Vijana wengi hujiuliza, naanzaje KUJITOLEA bila kulipwa chochote? Jibu ni rahisi kabisa, anza kujiangalia una ujuzi/kipaji gani? Pia angalia changamoto zilizopo kwenye jamii…FIKIRI kwa makini! Unaweza kufanya nini kulingana na ujuzi au uwezo wako kutatua changamoto zilizopo.

Narudia tena FIKIRI! tena kwa mapana(Uwe na taswira kubwa) ANZA kidogo kulingana na uwezo wako ukizingatia kiasi kidogo cha pesa ulicho nacho.Tambua kuwa, mabadiliko makubwa huanzia na jitihada ndogo ya mtu mmoja. 
Chukulia mfano wa mtu kama Mahtma Gandhi alivyoweza kuleta mabadiliko makubwa nchini India.Alituachia msemo huu maarufu duniani  Be the change that you wish to see most in your world”-Mahatma Gandhi.-Uwe chanzo cha mabadiliko utakayo kuyaona.

ANZA SASA! kwa  kujiweka, kujitokeza sehemu zenye fursa ili uonekane…TAMBUA kuwa FURSA HAIKUTAFUTI! JITOKEZE KUONA FURSA! Soma hii. http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/09/somo-kupitia-mimeatafuta-fursa-uonekane.html

Huna sababu ya kutembea na bahasha au kushinda ukipezi kutafuta nafasi za kazi mtandaoni au magazetini.Tambua kuwa kazi nyingi hutolewa kwa kufahamiana.

Najua mwanzo mgumu! Fahamu kuwa hakuna kitu kinapatikana kiurahisi…ukiona kipo cha urahisi kina shaka! Ni lazima utalipia gharama…Waingereza wanasema  hivi “you will pay the price nothing is for free”

Nikutie moyo zaidi kijana uliyekata tamaa ya kupata ajira kupitia nukuu maarufu ya mwandishi na msemaji wa hadhara- Zig Ziglar anasema(na si alisema, kwa sababu maneno yake yanaishi)  “You will get all you want in life if you help enough other people get what they want”- Zig Ziglar.(Utapata ukitakacho maishani kwa kuwasaidia wengine kikamilifu kupata wanachotaka).

Angalizo:
  • Usisahau kuwa Jielimishe Kwanza! inahitaji watu wa kujitolea "Volunteers" katika njanya ya Uandishi wa makala zenye mtazamo chanya na kuhamasisha utendaji bora wa kazi.
Tuwasiliane:          0716 075 826                                              jielimishekwanza@gmail.com

Imetayarishwa na kutolewa na






Jumapili, 6 Oktoba 2013

BIASHARA: MJUE MPINZANI WAKO KATIKA BIASHARA…BORESHA UBORA NA THAMANI!


B
iashara hujumisha kuuza na kununua kwa lengo la kupata faida…kwa muuzaji na pia mnunuzi anafaidika kwa kupata thamani (kwa lugha ya Kiingereza hujulikana kama “value”) ya huduma au bidhaa aliyoilipia. Ifahamike kuwa mteja/mnunuzi huridhishwa na thamani-“value” ya huduma au bidhaa, hivyo kutoa pesa yake kununua/kulipia gharama ya bidhaa/huduma inayotoa/kuleta thamani kwake.
Hapa ndipo inapotumika kanuni rahisi ya Uchumi inayosema; watu hulipwa kwa kuleta uthamani katika soko “people get paid by bringing value to the market place”.Itambulike kuwa kuna njia mbali mbali ambazo mtu anaweza kulipwa kwa kuleta uthamani katika soko.Mfano: kupitia biashara na kuajiriwa.
Siku zote Wafanyabiashara wanaitumia sana kanuni hii ya “kulipwa kupitia uthamani na ubora wauletao katika soko” kwa kujua au kutokujua hasa kwa kujilinganisha na wapinzani wao wa biashara na kuboresha mapungufu au udhaifu wa wapinzani wao.
Ni vyema na ni wajibu kumjua mpinzani wako na kumfuatilia kwa ukaribu sana na si kumchukia, kumfanyia mizengwe au kumpotezea. Kuthibitisha hilo angalia mfano wa wapinzani hawa wa biashara jijini Dar es salaam nchini Tanzania...

Kila mmoja anamtumia mwenzie kwa lengo zuri la kuleta uthamani wa huduma aitoayo kwa mtumiaji/mteja.Mwisho wa yote ni kazi ya mtumiaji kuchagua.
Mtambue mpinzani wako, mfuatilie kwa umakini bila kuiga kila kitu anachofanya…wewe boresha ubora wa huduma/bidhaa yako utafanikiwa.
Pia soma hii http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/08/biashara-ukitaka-kujenga-biashara-imara.html    na

http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/06/biashara.html
Imetayarishwa na kutolewa na






Alhamisi, 3 Oktoba 2013

UKITAKA KUFANIKIWA KIMAISHA JIEPUSHE NA MARAFIKI WA AINA HII


Mafanikio ya mtu yapo mikononi mwake, pia ni jinsi anavyojitazama kwa mtazamo wa wengine na kujichukulia bila kuangalia wengine wanasemaje kuhusu maamuzi yake.
Mwanadamu ana nguvu ya asili ya kufanya machaguo.Nikimnukuu Hayati Baba wa Taifa la Tanzania- Mwalimu Julius K.Nyerere aliwahi kusema-Maisha ni kuchagua.Inategemea unaamua kuchagua nini kwa vile unavyotaka uwe. Jinsi ulivyo sasa kimaisha ni kutokana na maamuzi/machaguo yaliyofanyika siku zilizopita. 

Tunaweza pia kuchagua marafiki ili tushirikiane katika kupambana na changamoto za maisha.Marafiki hao wanaweza kuchangia au kudidimiza mafanikio yako kama umakini hautachukua nafasi yake.Inategemea ni aina gani ya rafiki unachangamana naye.Leo naomba nikujuze aina ya marafiki unaopaswa kujiepusha nao.Utawatambua kwa maneno yao na mazoea yao/tabia zao.

1.MARAFIKI WASIOTAKA KUELEZA YAO…ILA WANA UCHU WA KUJUA YAKO
Aina hii ya marafiki ni hatari sana…mara nyingi hukudodosa kujua mipango yako, mwisho kukukatisha tamaa, wakati huo huo wanatumia mawazo yako waliyoyabeza!

2.RAFIKI ANAYEJIJALI YEYE TU…HAJALI MUDA, MCHANGO WAKO
Hii ni hali ya ubinafsi inayoweza kuufanya urafiki uwe wa upande mmoja.Pia kupelekea mmoja kujiona ni zaidi kuliko mwingine.(Itambulike kuwa urafiki ni kufaidiana na kusaidiana…kila mmoja ana mtegemea mwenzake).

3. MARAFIKI WAENDEKEZA STAREHE KULIKO KAZI
Waepuke marafiki wavivu wasiopenda kufanya kazi na mwisho wa siku wanataka mtoke mkatumie ulizozichuma.Kundi hili litakurudisha nyuma kimaendeleo.Na kundi hili linalokuwa la kwanza kukukimbia ukiishiwa.Hakuna urafiki wa kweli kwenye kundi hili!

4. RAFIKI ANAYESEMA YAKO YA SIRINI KWA WENGINE
Muogope rafiki ikiwa umembaini! Huyu aweza kuwa mchonganishi.Unajua kuwa watu wengine wakielezwa siri huwa inawawasha miyoni mwao…hivyo huileza kwa wengine kirahisi sana.Mtambue rafiki wa aina hii…epuka kumueleza siri zako!

5.RAFIKI ANAYEPENDA KUKUKOPA HALAFU HAKULIPI…UKIMDAI UGOMVI MKUBWA!
Kundi hili hupenda kutumia njia ya urafiki kujineemesha kirahisi wakati huo huo likileta ugomvi ndani ya urafiki.Ukiiona umemkopesha rafiki yako pesa halafu amekaa kimya hadi siku aliyoahidi kukulipa ujue…………..ukitaka msigombane usidai! Ila ujue kuwa anakurudisha nyuma kimaendeleo, si unajua tena pesa haitoshi!


Picha na thechive.com


                                          Imetayarishwa na kutolewa na


Huu ni mtazamo wa Jielimishe Kwanza! Ukiiona kuna tabia nyingine waliyo nayo marafiki wa kuepukwa usisite kutuandikia na tutaiongezea kama kawaida…