-->
Ni dhahiri na ukweli usiopingika kuwa watu
wengi wanaamini kuwa ni elimu pekee ndiyo mkombozi na chanzo cha furaha
maishani.Ikiwa ni sanjari na msemo wa Kiswahili usemao; “Elimu ni ufunguo wa maisha” yaani bila elimu hujafungua maisha au
…! Bila shaka unakubaliana na dhana hii.
Wanafunzi kuanzia ngazi ya awali hadi chuo
kikuu wanasoma sana na hatimaye wanapofika mwisho wa safari yao huanza
kulinganisha walichojifunza na maisha halisi na mwisho wa siku tunajikuta tuna
makundi tofauti tofauti yenye mtazamo tofauti tofauti kwa mfumo ule ule wa
elimu:
·
Wengine huona kama wamepotea njia,
·
Wengine huanza kushtuka kuanza kuchagua kitu cha
kufanya wakiwa wamehitimu
·
Wengine hujitamba kuwa wana vyeti vizuri na
kujitukuza…hivyo kuchagua aina ya kazi
·
Wengine huanza kutumia kile walichosomea kutatua
matatizo katika jamii kiuhalisia
· Wengine hufurahia kutumia walichosomea kupanda
vyeo sambamba na ngazi za mshahara
·
Wengine hutumia elimu ndogo waliyo nayo kupewa
kazi wasizoweza kuzimudu
·
Wengine, wamethubutu kuviongezea vyeti vyao
uwezo kwa kuambatanisha na vya watu wengine kupata ajira zinazofahamika kuwa na
maslahi
…ndiyo hivyo, utaamua mwenyewe kujiweka
kwenye kundi ulipendalo!
Swali
la msingi
Naomba ujiulize, unakitumia kile
ulichokisomea kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu? au ilikuwa ni kwa ajili
ya kupata cheti tu au heshima isiyo na faida?
Hivi ina faida gani kusomea taaluma fulani
kwa miaka 3 au 4 au 5 halafu isitumike kuboresha utendaji au kutatua matatizo
katika jamii? Kwa mtazamo mwingine ni sawa na kupoteza muda na rasimali pesa ya
Taifa.
Hivi tukitafakari kwa kina, nini lengo kuu la
elimu? Ninaweza kuanisha malengo kadhaa ya elimu
·
Kuchochea na kukuza vipaji…elimu inapaswa
kuchochea/kukuza vipaji na si kudumaza vipaji
·
Kuboresha mtazamo wa kufikiri na kutenda hasa
katika kutatua matatizo ndani ya jamii
· Kumpa mtu ujuzi wa kufanya kazi kutegemeana na
kipaji chake…je unafanya kazi kulingana na kipaji chako?…au bora mkono uende
kinywani?
·
Kujenga mahusiano mema, ushirikiano na watu wa
jamii tofauti tofauti
·
Kumkomboa mtu na utumwa wa fikra…kumfanya mtu
kuwa huru kifikra
Nini
tufanye ili kuitendea haki elimu tuipatayo shuleni kwa manufaa ya jamii nzima
hasa ile iliyokosa fursa adimu ya kupata elimu?
Kuna manung’uniko kila kukicha kuhusu ukosefu
wa ajira…lawama zote hutupiwa serikali…hivi serikali ni nani? Bila shaka
utajibu kuwa ni watu, na watu wenyewe ni kama wewe na mimi!
Inasemekana, serikali pekee ndiyo yenye jukumu
la kutengeneza ajira.Sasa umefika wakati kwa wahitimu wa vyuo vikuu na
wanajamii kwa ujumla kutengeneza ajira na si kuitegemea serikali
pekee…nikuahakikishie hata ungekuwa wewe madarakani usingefanikiwa kumpatia
kila raia ajira anayoitaka kwa wakati anaotaka!
Tunapaswa kutumia tulichokisomea na vipaji
vyetu kutatua matatizo katika jamii kwa kuongeza fursa za ajira kwa wengine.
Education is not the learning of facts, but the training of mind to think -Albert Einstein
Huu ni mtazamo tu wa Jielimishe Kwanza!
Ikiwa una maoni au ushauri,
Usisite kutuandikia kupitia: